Kikunde ni kata ya Wilaya ya Kilindi katika Mkoa wa Tanga, Tanzania.

Kata ya Kikunde inajumuisha vijiji vya Kikunde, Mafulila, Ludewa na Mjimpya. Kata ya Kikunde ya awali imegawanywa na kufanya kuwa kata mbili tofauti, ambapo kata mpya ya Tunguli imeanzishwa, mnamo mwaka 2011, na kata hiyo ina vijiji vifuatavyo: Tunguli, Manyinga, Mtolo, Msamvu, na Lusane.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 16,621 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 10,468 waishio humo[2].

Wakazi wake ni wakulima na wafugaji wakiwa Wakaguru, Wanguu na Wamasai. Mazao ya chakula ni mahindi, maharage, mihogo na mbaazi. Kata hii ni maarufu kwa matunda aina ya maembe.

Wananchi wa kata hii hawana zao maalum za biashara isipokuwa maharagwe na maembe wakati wa msimu. Kwa wafugaji huuza mifugo yao katika mnada wa kila mwezi mara moja uliopo Kikunde.

Madini ya dhahabu ni utajiri uliogunduliwa hivi karibuni katika vijiji vya Mafulila. Kata hii ina misitu ya hifadhi na miti ya mbao.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Tanga - Kilindi DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-17. 
  Kata za Wilaya ya Kilindi - Mkoa wa Tanga - Tanzania  

Bokwa | Jaila | Kibirashi | Kikunde | Kilindi | Kilwa | Kimbe | Kisangasa | Kwediboma | Kwekivu | Lwande | Mabalanga | Masagalu | Mkindi | Msanja | Mvungwe | Negero | Pagwi | Saunyi | Songe | Tunguli


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kikunde kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.