Tunguli ni kata ya Wilaya ya Kilindi katika Mkoa wa Tanga, Tanzania. Kata hiyo imeanzishwa mnamo mwaka 2011, na ina vijiji vifuatavyo: Tunguli, Manyinga, Mtolo, Msamvu, na Lusane.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 10,902 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,774 waishio humo[2].

Jamii yake hujihusisha sana na kilimo cha mahindi, maharagwe, kwa wingi; pia wana kilimo cha mazao jamii ya mbaazi. Wakazi hao pia hujihusisha na ufugaji wa mbuzi, ng'ombe na kondoo.

Kata ya Tunguli ina shule za msingi nne, ambazo ni: Mjimpya, Lusane, Manyinga, na Tunguli. Pia ina shule moja ya sekondari ya Tunguli, lakini bado jitihada zinaendelea ili kuongeza shule ya pili.

Kituo cha afya cha Tunguli kinachomilikiwa na kanisa la Anglikana kinahudumia kata nzima na nyingine.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. Sensa ya 2012, Tanga - Kilindi DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-17.
  Kata za Wilaya ya Kilindi - Mkoa wa Tanga - Tanzania  

Bokwa | Jaila | Kibirashi | Kikunde | Kilindi | Kilwa | Kimbe | Kisangasa | Kwediboma | Kwekivu | Lwande | Mabalanga | Masagalu | Mkindi | Msanja | Mvungwe | Negero | Pagwi | Saunyi | Songe | Tunguli


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tunguli kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.