Kilao
Kilao ni lugha ya Kithai-Kadai nchini Laos, Vietnam na Kamboja inayozungumzwa na Walao. Mwaka wa 2005, idadi ya wasemaji wa Kilao nchini Laos imehesabiwa kuwa watu zaidi ya milioni tatu. Pia kuna wasemaji 18,500 nchini Kamboja (2009) na 10,000 nchini Vietnam (2007). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kilao kiko katika kundi la Kithai cha Kusini-Magharibi.
Lugha ya Kilao ni lugha rasmi nchini Laos. Inaelekeana na lugha ya Kithai lakini huandikwa kwa alfabeti tofauti kidogo.
Viungo vya nje
hariri- lugha ya Kilao kwenye Multitree
- makala za OLAC kuhusu Kilao
- lugha ya Kilao katika Glottolog
- lugha ya Kilao kwenye Ethnologue
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kilao kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |