Kipanya manyoya-mororo

Kipanya manyoya-mororo
Kipanya manyoya-mororo wa Dalton nchini Mauritania (Praomys daltoni)
Kipanya manyoya-mororo wa Dalton nchini Mauritania (Praomys daltoni)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Nusuoda: Myomorpha (Wanyama kama panya)
Familia: Muridae (Wanyama walio na mnasaba na panya)
Nusufamilia: Murinae (Wanyama wanaofanan na vipanya-miiba)
Jenasi: Praomys
Thomas, 1915
Ngazi za chini

Spishi 8:

Vipanya manyoya-mororo ni wanyama wagugunaji wa jenasi Praomys katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae wanaotokea katika misitu minyevu ya Afrika kusini kwa Sahara.

Maelezo

hariri

Panya hawa wana manyoya mororo ambayo yanaweza mafupi au marefu. Pua ni ndefu na masikio ni makubwa na ya mviringo. Urefu wa mwili ni mm 90-140, urefu wa mkia ni mm 110-170 na uzito ni g 12-70. Rangi yao ni njano, hudhurungi, kahawianyekundu au kijivu mgongoni na nyeupe au njano tumboni.

Wanapatikana katika misitu minyevu na hukiakia usiku. Hutumia sehemu ya wakati wao katika miti na hujenga viota kwa majani pia mitini au ardhini, pengine katika vishimo. Hula matunda, mbegu na sehemu kijani za mimea, na wadudu pia.

Spishi

hariri