Kitendawili cha Samsoni

Kitendawili cha Samsoni kinapatikana katika Kitabu cha Biblia cha Waamuzi ambacho kimejumuishwa katika simulizi kubwa zaidi kuhusu Samsoni, hakimu wa mwisho wa Waisraeli wa kale. Kitendawili ambacho Samsoni anakitumia kuwapa changamoto wageni wake thelathini wa harusi, ni kama ifuatavyo: "Kutoka kwa mlaji kikatoka kitu cha kula, na kutoka kwa mwenye nguvu kikatoka kitu kitamu."

Sikukuu ya Harusi ya Samson, Rembrandt, 1638

Suluhisho laonekana haliwezekani kupatikana kwa njia ya mkato peke yake, kwa kuwa linategemea uzoefu binafsi wa Samsoni, ambaye hapo awali alikuwa ameua simba dume na baadae kukuta nyuki na asali katika masalia ya simba huyo. Hata hivyo, waalikwa wa harusi wanachukua jibu kutoka kwa mke wa Samsoni; baada ya kupoteza dau, Samsoni anatakiwa kuwalipa wageni wake suti thelathini nzuri, ambazo anazipata kwa kuua watu thelathini.

Wachambuzi wa kisasa wamependekeza majawabu mengine ya kitendawili. Vipengele vya masimulizi yanayozunguka pia yamefasiriwa kwa njia mbalimbali, huku ulinganifu ukichukuliwa kutoka kwenye hekaya za Kigiriki za mashujaa waua-simba, na imani ya kale kwamba viumbe hai wangeweza kuibuka kutoka kwenye nyama mfu.

Masimulizi ya Biblia

hariri
 
Samson Akimchinja Simba, Doré

Hadithi ya kitendawili cha Samsoni inafanya sura ya 14 ya Kitabu cha Waamuzi. Inaanza wakati Samsoni anakutana na mwanamke Mfilisti katika jiji la Timna na kuamua kumwoa, kinyume na pingamizi la wazazi wake. Akiwa safarini kwenda Timna kukutana na mwanamke huyo, Samsoni anashambuliwa na mwana-simba. Roho wa Bwana anakuja juu yake, naye anamrarua simba kwa mikono yake mitupu.

Muda fulani baadaye, Samsoni anarudi Timna ili kumwoa yule mwanamke Mfilisti. Akiwa njiani, anapita mahali alipoua simba, na kubaini kuwa kundi la nyuki limeunda mzinga ndani ya masalia ya simba yule. Samsoni akakusanya asali kutoka kwenye mzinga kwa ajili yake na wazazi wake, lakini hawaambii wazazi wake kuhusu simba huyo.

Katika karamu ya harusi, Samsoni anatoa fumbo lifuatalo kwa wageni wake Wafilisti: [1]

Kutoka kwa mlaji kimetoka chakula na ndani ya yule mwenye nguvu kimetoka kitu kitamu.

Samson anadhani kuwa Wafilisti hawataweza kubahatisha jibu la kitendawili hicho ndani ya siku saba (kipindi cha karamu); dau la kitendawili ni vitambaa thelathini vya hariri na mavazi thelathini.

Wafilisti wakamlazimisha mke mpya wa Samsoni awasaidie katika kugundua jibu, wakimtishia kumchoma moto na kuiunguza nyumba ya baba yake kama atashindwa.

Mke akambembeleza Samsoni vilivyo ili ampe jibu la kitendawili, na katika siku ya saba Samson anasalimu amri kwa mkewe.

Mke wa Samsoni akapeleka jibu kwa wale wageni wa harusi, nao wakampa Samsoni jibu la kitendawili chake kabla ya jua kutua katika siku hiyo ya saba; wakisema: "Ni nini kilicho tamu kuliko asali? Na ni nini kilicho na nguvu kuliko simba?" [2] Samsoni anajibu: "Kama hamngelima na ndama wangu, hamngelitegua kitendawili changu." [2]

Roho wa Bwana anamjia Samson kwa mara nyingine na anaondoka kwenda Ashkeloni na kuwaua Wafilisti thelathini, akichukua mavazi yao kulipia deni analodaiwa na wageni wa harusi. Kisha, akiwa amekasirishwa na usaliti wa mkewe, Samsoni anarudi nyumbani kwao na yule mwanamke anatolewa kwa mgeni mmojawapo. Tukio hili lawa chanzo cha mfululizo wa mikingamo mingi hatarishi kati ya Samsoni na Wafilisti, kama inavyoelezwa kwenye aya zilizofuatia.

Marejeo

hariri
  1. Judges 14:14:NKJV (NKJV). Bible Gateway.
  2. 2.0 2.1 Judges 14:18:NKJV (NKJV). Bible Gateway.
  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitendawili cha Samsoni kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.