Kivuli cha mvua ni hali ya eneo ambalo liko nyuma ya mlima ambako mvua hainyeshi. Upande huu wa mlima unaitwa demani (usio na upepo). Upepo wenye unyevu ndani yake ukisukumwa dhidi ya mlima unapaswa kupanda juu ambako halijoto inashuka. Hewa baridi haiwezi kushika ndani yake kiwango cha mvuke wa maji sawa na hewa joto.

Picha ambayo ina upepo unavuma mlima. Maji huanguka nje na hukausha hewa. Wakati hewa inakwenda chini upande mwingine, huwasha moto, hushikilia maji na haina mvua.

Kadiri hewa yenye mvuke inavyopaswa kupanda juu, inapoa na mvuke unaanza kutona na kuwa maji yaani mvua inanyesha.

Hii ndiyo sababu ya kuwa milima mara nyingi huwa na upande mbichi wenye mvua nyingi na uoto mnene, ilhali upande wa demani (usiotazama upepo) mara nyingi ni kavu zaidi ikiwa na uoto mchache.

Mfano katika Afrika ya Mashariki ni Mlima Kilimanjaro: upande wa Moshi (Tanzania) hupokea upepo kutoka Bahari Hindi na mvua nyingi mnamo milimita 2,400 kwa mwaka; kinyume chake upande wa Kenya upo demani na hapa ni pakavu, mvua ni milimita 800 pekee.

Milima inazuia kifungu cha mifumo ya hali ya hewa inayoleta mvua na hutupa "kivuli" cha ukavu nyuma yake.

Kama inavyoonyeshwa na mchoro wa kulia, hewa ya joto yenye unyevu inayofika kwenye mtelemko wa mlima husukumwa na upepo uliopo juu ya kilele cha milima. Wakati inapofanya hivyo, inapoa, maji yake hunyesha kama mvua kabla ya kuvuka juu. Hewa, bila unyevu mwingi uliobaki, inaendelea juu ya milima lakini upande mwingi haina uwezo kunyesha mvua tena, maana hapa kipo "kivuli cha mvua".

Maeneo ambako kivuli cha mvua huwa na athira kubwa ni nyanda za juu za Tibet nyuma ya milima ya Himalaya, mbuga ya Patagonia nyuma ya milima ya Andes na Dekkani kwenye Bara Hindi iliyopo nyuma ya Ghat ya Magharibi.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.