Mbuga ya Patagonia

Mbuga ya Patagonia (pia Jangwa la Patagonia) ni eneo kubwa lenye tabianchi yabisi yaani kavu likiwa na kilometa za mraba 673,000. Linapatikana katika Patagonia ambayo ni sehemu ya kusini ya Argentina. Upande wa magharibi unapakana na milima ya Andes na upande wa mashariki na Bahari Atlantiki.

Sehemu ya jangwa magharibi mwa Mbuga ya Patagonia, ambako mvua inazuiwa na milima ya Andes.

Tabianchi inabadilika kutoka magharibi kwenda mashariki. Eneo lote liko kwenye kivuli cha mvua cha milima ya Andes ambayo inalazimisha upepo kutoka Pasifiki kuachana na mvua yake upande wa magharibi; kwa hiyo sehemu za magharibi karibu na milima ni kavu zaidi, wakati mwingi chini ya milimita 100 za mvua kwa mwaka. Sehemu hizo zinaonyesha tabia ya jangwa kabisa. Kadiri Patagonia inavyoenea upande wa mashariki na kukaribia Atlantiki, mvua huongezeka kiasi, ingawa hata upande huo si zaidi ya milimita 300 kwa mwaka. Kadiri usimbishaji unavyoongezeka, uoto unabadilika kuwa na vichaka hadi mbuga ya nyasi. [1]

Upepo mfululizo kutoka magharibi, upande wa Pasifiki, unakausha ardhi.

Upande wa kaskazini jangwa linabadilika polepole kuwa mbuga inayoitwa pampa katika Argentina.

Tanbihi

hariri
  1. The Physical Geography of Patagonia and Tierra del Fuego. Andrea M. J. Coronato, Fernando Coronato, Elizabeth Mazzoni and Mirian Vazquez
  Makala hii kuhusu maeneo ya Argentina bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mbuga ya Patagonia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.