Andes ni safu ya milima kunjamano na safu ndefu kabisa ya milima duniani. Inaendana na urefu wote wa Amerika Kusini upande wa magharibi wa bara hili, ikiongozana na mstari wa pwani ya Pasifiki kutoka Kolombia katika kaskazini hadi Chile katika kusini. Urefu wa safu yote ni takriban km 7,500. Milima ya juu inafikia kimo cha m 6,962 na wastani wa milima yote uko kwenye m 4000. Upana wa milima hii ni kati ya km 200 na 600.

Safu za milima ya Andes zinavyoonekana kutoka angani

Safu za milima na nyanda za juu

hariri

Ndani ya Andes kuna hasa safu mbili zinazokwenda sambamba kandokando lakini kuna pia sehemu ambako safu zimeongezeka kuwa zaidi ya mbili. Hizi safu kuiu ni "Cordillera Oriental" (kwa Kihispania maana yake ni safu ya mashariki) na "Cordillera Occidental" (safu ya magharibi); kati ya safu za pembeni kuna ile ya Cordillera de la Costa (safu ya pwani) nchini Chile. Katika sehemu ya katikati safu hizi zinazunguka nyanda za juu za Altiplano za Peru na Bolivia.

Nchi za Andes

hariri

Nchi saba za Amerika kusini zina sehemu za maeneo yao katika Andes: Kolombia, Ekuador na Venezuela katika kaskazini; Peru na Bolivia katikati, halafu Argentina na Chile katika kusini.

 
Licancabur, Bolivia/Chile
 
Llullaillaco, Chile/Argentina
 
Chimborazo, Ecuador
 
Cono de Arita, Salta (Argentina)

Milima mirefu

hariri

Milima mirefu zaidi iko katika kaskazini ya Chile na Argentina, halafu katika Peru, Bolivia na Ekuador.

Mlima mrefu kabisa ni Aconcagua katika Argentina kwenye mpaka wa Chile ambao ni mlima mrefu wa Amerika yote.

Volkeno

hariri

Andes zina volkeno nyingi kwa sababu ziko sehemu ya "mviringo wa moto" unaozunguka Pasifiki yote. Bamba la Nazca linajisukuma chini ya bamba la Amerika Kusini na kusababisha kukunjwa juu kwa safu za Andes. Magma hupanda juu kwenye mstari wa kuzama kwa bamba la Nazca hulisha volkeno. Andes ni mahali pa volkeno za kimo kikubwa duniani.

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Andes kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.