Kiyirrk-Mel (pia Kiyirrk-Thangalkl au Kidangedl) kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wayirrk-Mel katika jimbo la Queensland. Tangu mwanzoni mwa karne ya 20, wasemaji wa Kiyirrk-Mel walibadilisha lugha yao na kutumia Kiyir-Yoront badala ya lugha yao. Wengine hudai bado kuna wasemaji wachache, wengine husema kuwa hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kiyirrk-Mel, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiyirrk-Mel kiko katika kundi la Kipama cha Pwani. Wengine hukiangalia kama lahaja tu ya Kiyir-Yoront.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiyirrk-Mel kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.