Milima ya Kunlun
(Elekezwa kutoka Kunlun Mountains)
Milima ya Kunlun (kwa Kichina: Kunlun Shan) ni safu ya milima nchini China yenye kimo cha mita 3,000 hadi 7,000. Mlima mrefu zaidi ni Liushin Shan inayofikia mita 7,167. Kuna pia volkeno nyingi, mlipuko wa mwisho ulitoka mwaka 1951.
Kunlun ni safu ndefu sana ya milima inayoenea kwa kilomita 3,000 ikiwa mwisho wa nyanda za juu za Tibet upande wa kaskazini. Hivyo inapakana na Jangwa la Taklamakan upande wa kusini. Upande wa magharibi inapakana na milima ya Pamir, upande wa mashariki inaishia China ya Kati.
Marejeo
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Milima ya Kunlun kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |