Lacrosse ya wasichana

Kigezo:Hamisha

Msichana anacheza lacrosse.

Lacrosse[1] ni mchezo ambao unapendwa sana Marekani. Ni maarufu katika pwani ya mashariki ya Amerika katika majimbo kama New Jersey, New York, na Maryland. Mchezo ulichezwa na watu wasio na imani huko Amerika na Kanada. Michezo imekuwa maarufu katika majimbo ya magharibi mwa Amerika. Leo, mchezo unachezwa na wavulana na wasichana. Wasichana kutoka shule ya msingi hadi shule ya upili wanacheza lacrosse. Mchezo unachezwa katika masika. Lakini, wachezaji wengi wa kike wanacheza mwaka wote. Lacrosse ya wasichana ni kama soka lakini lacrosse inachezwa hewani.

Wachezaji wanashikilia fimbo, na fimbo ni kuni. Kuna mfuko mwishoni mwa fimbo. Wachezaji wanarusha, wanakamata, na wanadaka mpira mdogo. Mpira una ragi ya manjano. Wachezaji wa kike wanavaa jezi ambazo ni sketi ambazo ni rangi ya timu yao. Timu zinavaa sare. Pia, wasichana wanavaa miwani mikubwa ya kuhifadhi macho na mdomo wakati wa mchezo. Kwa viatu, wachezaji wanavaa raba. Wanacheza wakati wa hali ya hewa ya joto, lakini wakati wa baridi wachezaji wanavaa majaketi. Wachezaji hawawezi kuvaa vito wakati wa kucheza.  

Wachezaji wanajaribu kukamata mpira kwa fimbo zao. Kuna alama katika lacrosse ya wasichana. Mchezo unachezwa na timu mbili. Kila timu ina wachezaji kumi na mbili uwanjani. Kila timu inao makocha. Pia, kuna mchezaji anayecheza katika goli (mchezaji huyu ni golikipa). Kuna mwamuzi kwenye mechi. Kila msimu, timu itacheza kama mechi kumi na tano.

Timu itapata pointi inapofunga goli. Alama kawaida ni ya juu kama kumi hadi nane (10-8). Kawaida alama iko karibu. Wachezaji na timu zao wanashindana kushinda. Wanacheza dakika sitini. Mechi ina nusu mbili ambapo wachezaji wanacheza kwa dakika thelathini. Katikati ya kucheza, wachezaji wanapumzika kwa dakika kumi. Lakini, ikiwa watafungana, wachezaji na timu zao wanashindana kwa dakika sita zaidi. Mechi na mazoezi huchezwa kwenye uwanja wa nyasi, kawaida nje. Uwanja wa nyasi ni yadi mia moja. Wakati wote, wachezaji wanne na golikipa huwa nyuma ya mstari.

Kuna adhabu katika mchezo kama vile kusukuma, kuzuia, na kumgonga mchezaji kichwani. Wakati kuna adhabu, mpira hupewa timu nyingine au mchezaji anaondoka mechini. Kuna adhabu kwa sababu mchezo unaweza kuwa hatari.

Jina la mchezaji maarufu wa lacrosse ni Taylor Cummings. Alicheza lacrosse ya wasichana katika Chuo Kikuu cha Maryland. Yeye na timu yake walishinda sana ubingwa wa kitaifa. Pia, Taylor Cummings alishinda tuzo kwa kuwa mchezaji bora. Alishinda tuzo hii mara tatu. Taylo Cummings[2] alihitimu Chuo Kikuu cha Maryland katika 2016.

Tanbihi hariri

  1. "Women's lacrosse", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-11-16, iliwekwa mnamo 2019-12-04 
  2. "Taylor Cummings", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-07-31, iliwekwa mnamo 2019-12-04