Baikal

(Elekezwa kutoka Lake Baikal)

Ziwa Baikal (kwa Kirusi: Озеро Байкал = Osero Baykal) ni ziwa kubwa katika Siberia kwenye sehemu ya Kiasia ya Urusi. Baikal ni gimba kubwa la maji matamu duniani.

Ramani ya Baikal.
Ziwa la Baikal.
Samaki ya Omul sokoni.

Urefu wake ni km 636; upana km 20–80 na kina kirefu ni mita 1,600. Hakuna miji mikubwa kando ya ziwa lakini Irkutsk ni km 60 kutoka ziwani.

Ziwa hilo lina tabia za pekee. Aina 1600 kati ya aina 2,500 za wanyama na mimea za ziwa zinapatikana hapa tu. Nerpa ya Baikal ni sili ya pekee katika maji matamu; samaki ya Omul hupatikana hapa tu.

Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Baikal kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.