Ziwa Ontario
(Elekezwa kutoka Lake Ontario)
Ziwa Ontario ni moja kati ya maziwa makubwa ya Amerika ya Kaskazini. Ziwa limepakana na Kanada (Ontario) upande wa kaskazini halafu na Marekani (New York) upande wa kusini.
Jina la Ontario latoka katika lugha ya Kihurona likimaanisha ziwa kubwa.
Ziwa Ontario hupokea maji yake kutoka Ziwa Erie kupitia Mto Niagara. Maji hutoka kwa nia ya Mto Saint Lawrence.
Majiji mawili makuu ni Toronto (Ontario, Kanada) na Rochester (New York, USA).
Vipimo
haririZiwa lina urefu wa kilomita 311 na upana mkubwa wa 85 km. Uso wake una eneo la 19,500 km2. Kina cha wastani ni 86 m lakini kina kikubwa chafikia 244 m.
Maziwa Makubwa
hariri- Ziwa Superior
- Ziwa Huron
- Ziwa Michigan
- Ziwa Erie
- Ziwa Ontario
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ziwa Ontario kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |