Lango:Afrika/Makala iliyochaguliwa

Makala iliyochaguliwa hariri

Makala iliyochaguliwa kwa Aprili 2012 hariri

Faili:Askari.jpeg
Askari wa jeshi la kijerumani

Kampeni za Afrika ya Mashariki ulikuwa mfululizo wa mapigano ya kivita yaliyotokea Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (Tanganyika, Rwanda na Burundi ya leo) na koloni jirani za Msumbiji, Rhodesia ya Kaskazini (Zambia), Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (Kenya), Uganda, na Kongo ya Kibelgiji. Kampeni hizi zilianza mwezi wa Agosti 1914 zikaisha rasmi mnamo mwezi wa Novemba katika mwaka wa 1918. Wapiganaji katika vita hii walikuwa jeshi la kikoloni cha Kijerumani lililofanywa hasa na askari Waafrika waliosimamiwa na maafisa Wajerumani pamoja na walowezi Wajerumani na wanamaji wa manowari waliokaa Afrika ya Mashariki wakati wa mwanzo wa vita 1914. Dhidi yao walisimama jeshi dogo la kikoloni la Kiingereza katika Kenya na Rhodesia, halafu vikosi vya jeshi la kikoloni la Uhindi ya Kiingereza na vikosi kutoka Afrika Kusini.