Jimbo Katoliki la Zanzibar
Jimbo Katoliki la Zanzibar (kwa Kilatini "Dioecesis Zanzibarensis") ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania, likienea katika visiwa vya Unguja na Pemba vya Tanzania visiwani, jumla kilometa mraba 2,332.
Makao makuu yake ni katika mji wa Zanzibar na linahusiana na Jimbo kuu la Dar-es-Salaam.
Kanisa kuu limewekwa wakfu kwa heshima ya Mtakatifu Yosefu.
Askofu wa jimbo ni Augustine Ndeliakyama Shao, C.S.Sp.
Historia
haririUkristo ulianzishwa na wamisionari wa Shirika la Mt. Agostino kutoka Ureno walioongozana na Vasco da Gama mwaka 1499 hadi Zanzibar.
Huko walijenga konventi ya shirika lao ili kuhudumia kiroho Wakristo toka Ulaya tu.
Misheni ilipingwa na Waarabu Waislamu na kukoma mwaka 1698, kisiwa hicho kilipotekwa na Waarabu wa Oman.
Uinjilishaji ulianza upya katika sehemu ya pili ya karne ya 19 ambapo tangu mwaka 1860 Zanzibar ilikuwa makao makuu ya Vikarieti ya Kitume iliyoenea hata bara.
Jimbo liliundwa rasmi tarehe 28 Machi 1980 baada ya kujitegemea tangu 12 Desemba 1964 kama Apostolic Administration.
Takwimu
haririWaumini ni 12,794 (2010) kati ya wakazi 1,221,000 (sawa na 1%), wengi wao wakiwa Waislamu.
Mapadri ni 20, ambao kati yao 18 ni wanajimbo na 2 ni watawa. Hivyo kwa wastani kila mmoja anahudumia waumini 639 katika parokia 7.
Maaskofu
hariri- Edgard Aristide Maranta, O.F.M.Cap. † (12 Desemba 1964 - 1966 kujiuzulu)
- Joseph Sipendi † (1966 - 1968 kujiuzulu)
- Adriani Mkoba † (16 Julai 1968 - 26 Januari 1973 kujiuzulu)
- Bernard Martin Ngaviliau, C.S.Sp. † (28 Machi 1980 - 30 Novemba 1996 kustaafu)
- Augustine Ndeliakyama Shao, C.S.Sp., tangu 30 Novemba 1996
Viungo vya nje
hariri- www.catholic-hierarchy.org katika ukurasa [1]
- www.katolsk.no katika ukurasa[2]
- (Kiingereza) [3] kwenye www.gcatholic.com
- (Kiingereza) [4] Archived 26 Mei 2015 at the Wayback Machine. kwenye tovuti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
- Hati Quo aptius, AAS 57 (1965), uk. 336
- Hati Cum Administratio
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Zanzibar kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |