Leokrisya (alifariki Cordoba, Hispania, 15 Machi 859) alikuwa binti wa familia ya Kiislamu aliyeacha dini hiyo ajiunge na Kanisa Katoliki.

Mt. Leokrisya alivyochorwa akishuhudia kifodini cha Eulogi wa Cordoba.

Alipokamatwa nyumbani pamoja na askofu Eulogi wa Cordoba alikatwa kichwa na Waislamu waliotawala nchi hiyo kwa sababu alikataa katakata kurudi nyuma[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Machi[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Vyanzo hariri

  • Tolan, John, Medieval Christian Perceptions of Islam, New York: Routledge, 2000. ISBN 0-8153-1426-4

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.