Leonidas wa Aleksandria

Origen, mtoto wa Leonidas.

Leonidas wa Aleksandria (kwa Kigiriki: Λεωνίδης, Leonides; alifariki 202) alikuwa Mkristo wa Misri ambaye alifia dini yake kwa kukatwa kichwa wakati wa dhuluma ya kaisari Septimius Severus[1].

Leonidas alimsaidia mwanae Origen kujiendeleza kadiri ya akili yake kubwa ajabu na kujua Biblia tangu utotoni[2]. Baada ya huyo, alizaa walau watoto wengine sita[3].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu[4].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Aprili.[5]

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  1. Eusebius Pamphilius, Church History, Book VI, Chapter I
  2. Origen's father
  3. Crouzel, H. trans. A. S. Worrall, Origen (Edinburgh: T&T Clark, 1989)
  4. https://dacb.org/stories/egypt/leonides/
  5. Butler, A., Lives of the Saints: St. Leonides, Martyr, accessed 23 December 2016