Levy Mwanawasa (Mufulira, * 3 Septemba 1948 - 3 Julai 2008) alikuwa rais wa tatu wa Zambia tangu uhuru wa nchi.

Levy Mwanawasa, 2004

Alizaliwa katika Mufulira (Zambia). Akamwoa Maureen Mwanawasa katika ndoa yake ya pili akazaa naye watoto 4.

Mwanawasa alisoma sheria kwenye Chuo Kikuu cha Zambia akafanya kazi ya wakili tangu 1974. 1985 alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya Zambia kwa muda wa mwaka moja.

1991 aliteuliwa na rais Frederick Chiluba kama makamu wake. Akawa makamu wa rais lakini alianza kupinga kiwango kikubwa cha rushwa serikalini na mwaka 1994 akajiuzulu akarudi katika kazi ya mwanasheria.

2001 aliteuliwa kama mgombea wa MMD (Movement for Multiparty Democracy) akashinda ingawa alipata asilimia 29 ya kura tu katika sheria ya Zambia isiyo na kura ya pili. Mgombea wa pili wa upinzani Anderson Mazoka alimkaribia kwa asilimia ya 27 za kura zote akapinga matokeo akidai palikuwa na udanganyifu. Mahakama Kuu ikathebitisha uchaguzi hata ikikubali ya kwamba makosa yalitokea.

Mwaka 2006 Mwanawasa alirudishwa kama rais kwa safari ya pili.

Aliaga dunia tar. 3. Julai 2008 kwenye hospitali mjini Paris alipopelekwa baada ya kupigwa na kiharusi wakati wa kukudhuria kikao cha Umoja wa Afrika nchini Misri.