Kingala (Kongo)
Lugha ya Kibantu inayozungumzwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Kongo
(Elekezwa kutoka Lingala)
Kilingala (au Lingala) ni lugha ya Kibantu hasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako ni lugha ya taifa na Jamhuri ya Kongo ambako pia imetambulika rasmi. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kilingala kiko katika kundi la C40.
Kinazungumzwa hasa na Wangala.
Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kilingala kama lugha ya kwanza katika Jamhuri ya Kidemokrasia imehesabiwa kuwa zaidi ya watu milioni 5.5; pamoja na hayo kuna watu milioni saba ambao huongea Kilingala kama lugha ya pili. Tena kuna wasemaji wa Kingala nchini Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Gabon, Guinea ya Ikweta, Kamerun, Chad na Angola.
Viungo vya nje
hariri- lugha ya Kilingala kwenye Multitree
- makala za OLAC kuhusu Kilingala Ilihifadhiwa 24 Juni 2013 kwenye Wayback Machine.
- lugha ya Kilingala katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/lin
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kingala (Kongo) kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |