Lugha ya kwanza
Lugha ya kwanza ni lugha ambayo mtu anaiongea kama lugha yake ya kwanza tangu utotoni, umri ambamo ni rahisi zaidi kuathiriwa na mazingira na hivyo pia kujifunza kusema kama watu wa kandokando.
Pia lugha hiyo huitwa lugha mama (kwa Kiingereza "mother tongue") kwa vile watu wengi hujifunza lugha yao ya kwanza kutoka kwa mama mzazi. Lakini hiyo si lazima: mara nyingine mtoto halelewi na mama, au kama analelewa, anatumia muda mrefu zaidi na watoto wenzake (hasa shuleni), hivyo anazoea lugha yao kuliko ile ya nyumbani, hata kama ni tofauti kabisa.
Kwa sababu hiyohiyo wapo watu wenye lugha mama zaidi ya moja.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lugha ya kwanza kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |