Ludolfo, O.Prem. (alifariki Wismar, Holstein, Ujerumani, 1250) alikuwa askofu wa Ratzeburg kutoka shirika la Wapremontree, ambaye, kwa sababu ya kutetea uhuru wa Kanisa alitupwa katika gereza duni sana kwa amri wa mtemi Alberto I wa Saxony; huko alidhoofika kiafya, kiasi kwamba alipotolewa kifungoni akafariki dunia mara moja[1].

Mt. Ludolfo (kushoto), pamoja na Wat. Evermodo na Isfridi.

Ndiyo sababu tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Machi[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.