Unestori : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|Nestori kadiri ya [[Romeyn de Hooghe (1688)]] '''Unestori''' (kwa Kiingereza Nestorianism<ref>[http://www.ec-p...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 12:57, 10 Oktoba 2017

Unestori (kwa Kiingereza Nestorianism[1]) ulikuwa tapo la Ukristo lililofuata mafundisho ya Nestori, mmonaki na mwanateolojia aliyefikia kuwa Patriarki wa Konstantinopoli (leo Istanbul) tangu tarehe 10 Aprili 428 hadi Agosti 431, ambapo kaisari Theodosius II alithibitisha uamuzi dhidi yake uliopitishwa na Mtaguso wa Efeso tarehe 22 Juni.

Nestori kadiri ya Romeyn de Hooghe (1688)

Kwa kukataa jina lililozoeleka la Θεοτόκος, Theotokos, "Mama wa Mungu", kwa Bikira Maria, Nestori alisababisha mabishano makubwa na hatimaye mafarakano kuhusu fumbo la Yesu Kristo.

Hasa Sirili wa Aleksandria alimpinga vikali kwa kudai haamini umungu wa Yesu, ingawa mwenyewe alizidi kujitetea hadi kifo chake kwamba anashika imani sahihi.

Matokeo ya mabishano hayo ni Kanisa la Asiria kutengana na Kanisa Katoliki hadi leo, ingawa kwa sasa mafundisho kuhusu Yesu yamelingana.

Tanbihi

  1. Nestorius Ecumenical Patriarchate

Vyanzo

Viungo vya nje

  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Unestori kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.