Bomu

(Elekezwa kutoka Mabomu)

Bomu (wingi: mabomu; kutoka Kiingereza "bomb") ni silaha inayoundwa kwa kilipukaji kama baruti, dainamiti au kemikali nyingine zinazoingia katika mchakato unaoachisha nishati nyingi haraka. Bomu ni silaha unayolenga kuleta uharibifu kwa njia ya mshtuko mkali. Mshtuko huu huleta wimbi kali ya hewa inayoweza kuua au kuumiza watu na kuvunja vitu. Mara nyingi uharibifu wa mlipuko wa bomu unakuja pamoja na vitu vinavyorushwa hewani kama risasi.

Mfano wa bomu.

Yamekuwa yakitumika kwa karne nyingi. Mabomu mengine hujengwa kwa kusudi la kurusha vipande vya chuma, na baadhi ni mabomu ya moto.

Mabomu mengi hayana nishati zaidi kuliko mafuta ya kawaida, isipokuwa katika kesi ya silaha ya nyuklia. Hata hivyo, hutoa nguvu zake kwa haraka zaidi, hivyo ni za hatari zaidi.

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.