Madhara yasiyokusudiwa

Madhara yasiyokusudiwa (kwa Kiingereza: collateral damage) ni istilahi ya kutaja tukio baya lisilokusudiwa.

Istilahi hiyo hutumika hasa katika maadili na katika tiba kuhusu uharibifu unaotokea wakati mtu analenga jambo jema, kama uponyaji wa mgonjwa. Mara nyingi dawa zinamsaidia kweli lakini kwa kiasi fulani zinamdhuru pia.

Kijeshi inamaanisha uharibifu wa mali za raia au watu majeruhi ambao si wapiganaji, yaani, raia wa kawaida tu.[1] Mfano ni wakati wa matumizi ya silaha kama mzinga, bomu au kombora dhidi ya wanajeshi adui: katika nafasi hiyo watu au nyumba za kiraia wanaweza kupigwa ama kwa kosa au kutokana na ukali wa mlipuko.

Marejeo

hariri
  1. "collateral damage". Merriam-Webster.

Viungo vya Nje

hariri