Jean de Dieu Makiese (28 Mei 1952 - 11 Agosti 2007), alifahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Madilu System, alikuwa mtunzi na mwimbaji wa muziki wa soukous. Alizaliwa huko mjini Léopoldville, enzi hizo iliitwa Kongo ya Kibelgiji - ambayo leo hii inajulikana kama Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Alipata kuwa mwanachama wa bendi ya soukous maarufu kama TPOK Jazz ambayo ilitamba sana katika tasnia ya muziki wa Kikongo katika miaka ya 1960 hadi 1980.[1]

Madilu System
Jina la kuzaliwaJean de Dieu Makiese
Pia anajulikana kamaMadilu Bialu
Amezaliwa(1952-05-28)Mei 28, 1952
Amekufa11 Agosti 2007 (umri 55)
Kazi yakeMtunzi, mpanga muziki, mtayarishaji wa rekodi, mwimbaji
AlaSauti
Miaka ya kazi1970 - 2007
Ameshirikiana naTPOK Jazz

Kazi ya muziki

hariri

Akiwa bwana mdogo mnamo mwaka wa 1969, Madilu aliimba na "Orchestre Symba", "Orchestre Bambula", iliyokuwa ikiongozwa na Papa Noel, na vilevile aliimba na "Festival des Maquisards", iliyokuwa ikiongozwa na Sam Mangwana. Madilu baadaye akaanzisha bendi yake mwenyewe iliyokuwa inajulikana kama "Orchestre Bakuba Mayopi".

Hata hivyo, haikutamba kivile hadi hapo alipoungana na Franco, hapo ndipo alipoanza kuwa mwimbaji maarufu sasa wa Kikongo na kuwa nyota maarufu wa Kimataifa. Franco ndiye aliyempachika jina la Madilu System, jina ambalo baadaye lilidumu. Kibao kikali cha kwanza cha Madilu akiwa na TPOK Jazz kilikuwa “Mamou (Tu Vois),” ambacho kilitamba sana mnamo mwaka wa 1984. Hilo lilipelekea Madilu kumiliki tungo yake mwenyewe katika bendi, “Pesa Position.” Baadaye ikaja “Mario” na “Reponse de Mario” mnamo mwaka wa 1985 na huenda hii ilikuwa moja kati ya kazi bab-kubwa zilizofanywa pamoja kati ya Franco-Madilu, “La Vie des Hommes” mnamo 1986.

Kufuatia kifo cha Franco, TPOK Jazz ilisimama kutengeneza muziki kwa muda wa mwaka mmoja. Kisha kundi likarudi tena lakini safari hii na Madilu akiwa kama kiongozi mkuu. Miaka iliyofuata, alikuwa kiungo kikuu cha bendi katika kuunganisha upya bendi, kote jukwaani na studio. Madilu baadaye akaenda kuanzisha bendi yake binafsi yenye mafanikio makubwa. Baadaye akahamishia makazi yake huko mjini Paris, Ufaransa na baadaye Geneva, Uswizi, huku akidumisha kikosi kikubwa cha mashabiki zake wa nyumbani huko mjini Kinshasa.

Mwanzoni mwa mwezi wa Agosti 2007, Madilu alisafiri hadi mjini Kinshasa kwenda kupiga video kwa ajili ya nyimbo zake mpya. Alianguka Ijumaa ya tarehe 10 Agosti, 2007. Alipelekwa katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Kinshasa, ambapo alifia asubuhi yake iliyofuata, Jumamosi ya tarehe 11 Agosti, 2007.[2]

Diskografia

hariri
Mchango wa msanii kwenye

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Obituary Archived 2012-07-11 at Archive.today, The Independent, 22 September 2007
  2. The Music Career of Madilu System

Viungo vya Nje

hariri