Majadiliano:Bumbuli

Latest comment: miaka 13 iliyopita by Muddyb Blast Producer in topic Historia ya Bumbuli

Historia ya Bumbuli hariri

Historia ya Bumbuli ni ndefu sana. Mimi nimeendeleza makala hii ya Bumbuli lakini kama kuna msambaa mwenzangu au mtu mwingine yeyote mwenye kujua mambo mengine kama majina ya Wamisionari wa Kijerumani waliojenga hospitali ya Bumbuli, Maajabu za Ziwa kubwa lililokuwa linaitwa Tighotwe ambalo kwa sasa ni uwanja wa mpira wa miguu n.k. Naomba tusaidiane kuboresha makala hii ya mji wetu wa Bumbuli. Shadrack Masaga.

Shadrack, mambo vipi! Ni matumaini yangu kuwa bomba sana. Haya, nimeona umeandika makala nyingi kutoka mjini Bumbuli, lakini pia zimekuwa makala za mbegu na zitahitaji maongezeo mengi tu. Wazo langu, unaonaje makala zile mbili tatu tusiziunganishe kwenye makala moja ya Bumbuli? Inakuwa rahisi kujenga vichwa vya uchawi na huku zake. Ukiwa tayari kwa hili, tafadhali jibu hapahapa na nitaanza kukuonesha namna ya kuanza! Kila la kheri. Wako,--MwanaharakatiLonga 06:17, 15 Septemba 2010 (UTC)Reply

Hallo Muddy mambo zako nadhani ni poa kabisa. Sasa labda kuna kitu sijakuelewa vizuri hapa, unamaanisha kuwa, kwa mfano suala la uchawi liunganishwe kwenye makala ya Bumbuli kama mbegu? au ulikuwa unamaanisha kitu gani? Naomba ufafanue kidogo swali lako ili tuweze kuboresha zaidi. Asante sana. Swala langu jingine ni kwamba nimefaulu kupakia picha kama ulivyoiona lakini process za kubadili picha bado sijaifahamu naomba unisaidie kwa hilo. Yaani kama hiyo picha iliyopo hapo nataka kuibadilisha na kuweka nyingine inakuwaje. Halafu pia nataka kuweka picha za historia sehemu ya historia za utawala sehemu ya utawala process yake inakuwaje? Nashukuru kwa msaada wako kwani nilikuwa mgeni sana kwenye wikipedia lakini unanitia moyo sana niendelee. Asante Shadrack

Return to "Bumbuli" page.