Wazo. Nimeona tatizo upande wa kutaja mwanamuziki na muziki. Kigezo hiki kinajumuisha mambo mawili kwa wakati mmoja. Yaani, mwanamuziki, single, bendi, na kadhalika. Sidhani kama ni wazo zuri kiasi fulani - hasa ikiwa tumeamua kutenganisha makala kwa mtililiko wa majina husika na tendo lenyewe. Nilifikiria kufanya hivi: "Makala hii kuhusu muziki/mwanamuziki fulani bado ni mbegu" badala ya hivi: "Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu". Sikuweka haya juu kwa kufuatia jamii inayoingiza mambo yote hayo ni moja: "Mbegu za wanamuziki" ilhali makala zingine si za wanamuziki, bali muziki au albamu ya muziki. Je, hii ni sahihi kuchanganya makala za muziki na wanamuziki? Wenu kijana mtiifu, Muddyb, au--Mwanaharakati (Longa) 07:11, 29 Juni 2009 (UTC)Reply
- Nimetofautisha vigezo vya mbegu za muziki na vigezo vya mbegu za wanamuziki. Asante kwa shauri zuri! --Baba Tabita (majadiliano) 13:39, 29 Juni 2009 (UTC)Reply
- Hongera pia kwa mabadiliko na ujenzi wote ulioufanya!--Mwanaharakati (Longa) 05:03, 30 Juni 2009 (UTC)Reply