Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Baba Tabita (majadiliano) 02:44, 18 Aprili 2015 (UTC)Reply

Kuhusu Maana hariri

Salamu, naona umeanzisha makala za MAANA,mfano ukachukua makala ya Jomo Kenyatta na Uhuru Kenyatta na kuziweka katika makala za MAANA, Je majina ya Jomo Kenyatta na Uhuru Kenyatta ni Majina yanayofanana ?. ingekuwa vyema kutafuta makala halisi zenye majina yanayofanana, mfano MOSHI,akama tunavyojua kuna Moshi eneo na ule unaotokana na kuungua kwa kitu,lakini kwa jinsi ulivyoweka wewe haifanani,tazama hapa Msaada:Maana, Amani Sana Idd ninga (majadiliano) 19:03, 8 Aprili 2023 (UTC)Reply

Salamu, bado unatumia MAANA hasa za majina ya watu,Je kuna umuhimu wowote wa kuweka majina hayo katika maana ihali ya kuwa ni majina tofauti ?, tukiangalia tunaweza kutumia neno kama KARO, kwa sababu kuna Karo lile la kuoshea vyombo na kuna KARO ile inayolipwa kama ada shuleni,maneno kama haya mawili tunaweza kuyatumia na kuyaweka sehemu ya maana, lakini kama tukitumia majina ya watu Mfano JOHN tukasema tuliweka katika maana, Tutaweka majina mangapi yanayoanziwa na John,umeona umuhimu wowote wa hiyo njia unayotumia ? Amani sana Idd ninga (majadiliano) 20:17, 18 Aprili 2023 (UTC)Reply
Tafadhali tujadiliane kwanza kabla ya kuendelea kuweka aina ya makala zako,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 15:02, 26 Aprili 2023 (UTC)Reply
Tafadhali, ukianzisha makala weka [[Jamii:majina]] na kiungo kwa lugha nyingine (interwiki). Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:49, 30 Mei 2023 (UTC)Reply