Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Kutaja vyanzo hariri

Ndugu nimeona ulileta makala ambazo nilipeleka katika ukurasa wetu ambako zitaangaliwa kama zinaweza kubaki au la. Angalia Wikipedia:Mwongozo_(Anzisha_makala) na hasa Wikipedia:Umaarufu . Sitaki kukukatisha tamaa, ukiwa na swali: karibu! Kipala (majadiliano) 14:11, 25 Agosti 2018 (UTC)Reply

Asante sana kwa bahati hii ya pekee ya kuweza kuleta historia na wasifu wa washairi na waandishi wa VITABU Tanzania.

naomba tuendelee kuvumiliana kidogo katika kipindi himi kwani kuna baadhi ya makosa ya kiuandishi hutokea.

naweza kuwasiliana nanyi moja kwa MOJA moja kwa barua pepe yangu ?
Sawa kabisa, ukienda ukurasa wangu utaona upande wa kushoto chini ya kichwa "Vifaa" kipengele "Email this user", hapa utanipata. Kipala (majadiliano) 13:28, 26 Agosti 2018 (UTC)Reply

Saadani Abdu Kandoro hariri

Asante kwa mchango kuhusu Saadani Kandoro, ni muhimu. Ila tu hatuwezi kuacha makala bila vyanzo na marejeo. Ulipata wapi matini zako? Lazima kutaja. Kipala (majadiliano) 12:58, 16 Septemba 2018 (UTC)Reply

JASHO LA MVUA hariri

Umeleta makala hii, mimi napendekeza kuifuta (lakinii una nafasi ya kuiboresha. Matini uliyoleta haifuati muundo wa makala, haitaji nani ni mwandishi na haielezi yaliyomo ya kitabu. Badala yake unaleta matini ya tangazo la biashara ya wachapiaji ambayo haikubaliki. Tumia muda unaobaki kabla ya kufutwa kwa makala!. Kipala (majadiliano) 19:57, 20 Aprili 2019 (UTC)Reply

Patrick Mfugale hariri

Asante kwa mchango huu wa maana. Ila tafadhali sana usimalize haraka. Jitahidi kuchungulia sentensi zako, na kuepukana na yale makosa mengi ya tahajia. Asante. Kipala (majadiliano) 21:05, 9 Februari 2020 (UTC)Reply

Kuboresha makala hariri

Ndugu, tunakushukuru kwa michango yako, ila angalia tunavyoirekebisha iwe bora zaidi. Naona unarudia makosa yaleyale, kumbe unaweza kutupunguzia kazi ya kuyarekebisha. Pembeni mwa mabadiliko ya karibuni angalia tofauti kati ya ulivyoandika wewe na ninavyorekebisha mimi. Wote tumejifunza hivi. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:31, 27 Februari 2020 (UTC)Reply

Mlima Kubi Gangri hariri

Asante kwa makala. Tafadhali maliza makala! Haina jamii, haina interwiki (kuunganisha na lugha nyingine). Pia inafaa kuangalia makala ya en.wiki na angalau kunakili kutoka pale vyanzo na marejeo. Kama una swali, uliza - usikae kimya. Hakuna maswali mabaya, lakini kuna makala mabaya shauri ya kutouliza swali! Kipala (majadiliano) 18:39, 5 Machi 2020 (UTC)Reply

Kinachokosekana ni jamii na interwiki.
Jamii: kwanza angalia makala ya enwiki inatumia jamii gani (kama makala ya enwiki ipo). Pale unaona "Categories: Mountains of Nepal,Mountains of the Tibet Autonomous Region,China–Nepal border,International mountains of Asia,Nepal geography stubs,Tibet geography stubs". Hapa utachagua, Hatuna jamii kuhusu mpaka ule, ningeacha. Vilevile hatuna "milima ya kimataifa..". Lakini nisipokosei tuna milima ya Nepal (kama bado: jiografia ya Nepal?), pia milima ya Tibet (?) au China. Lazima uangalie. Hakika tuna jamii:Himalaya. Inafaa. Hizi za "stubs" (=mbegu za...) mimi mwenyewe sianzishi kama haziko tayari.
Interwiki: tafuta jina la makala kwa Kiingereza. Halafu kwenye ukurasa wa makala mpya "Mlima Kubi Gangri" bofya chini kushoto hapa "Lugha - Ongeza viungo/Add links". Sasa fuata maelezo ya hapa: Wikipedia:Mwongozo_(Viungo_vya_Wikipedia).
Menginevyo ningeshauri fungua makala ya Kiingereza. Hatuwezi (bado) kunakili hiyo infobox na pia hatuwezi kuchukua ramani hii. Lakini unaweza kuchukua majiranukta. Bofya "Edit Source". Fungua pembeni makala ya Mlima Everest, bofya hariri chanzo, nakili sehemu yote ya majiranukta (coordinates), bandika ktk makala ya Mlima Kubi Gangri, sasa chukua namba kutoka coordinates ya enwiki na andika katika sehemu uliyonakili kutoka Everest.

Pia nakili sehemu ya "External links" kutoka enwiki, bandika sw. BAsi hii itoshe nitaangalia kesho ulifika wapi. Wasalaam. Kipala (majadiliano) 19:22, 5 Machi 2020 (UTC)Reply

Mtumiaji:Idd Ninga hariri

--Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:39, 22 Aprili 2020 (UTC)Salamu, Hongera kwa kuendeleza michango yko katika sw.wiki ni vyema uandike chochote katika ukurasa wako wa mtumiaji. 196.41.58.174 19:10, 11 Machi 2020 (UTC)Reply

Idd habari naomba uwasiliane nami kwa barua pepe kupitia "email this user" ukiangalia ukurasa wangu wa mtumiaji (bofya chini kwa jina langu, menyu "Vifaa" upande wa kushoto, nafasi ya sita kwenye menyu ).
Tukiwasiliana kwa email kupitia wikipedia, anwani haionyeshwi kwa hiyo ni siri yako na yangu.
Naona unafanya mengi na hapa nafurahi. Naona pia unahitaji bado ushauri maana kuna kasoro ambazo si lazima, sina shaka kwamba unaweza kushika haraka na kuboresha makala zako. Kipala (majadiliano) 16:53, 14 Machi 2020 (UTC)Reply

Tangazo hariri

Habari ndugu Mwanawikipedia!

Mimi ni mwezeshaji wa mradi uitwao Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Ni mradi mchanga/mpya ambao Shirika la Wikimedia Foundation linanuia kuuanzisha endapo wadau wataona ni mradi unaofaa. Nakukaribisha usome mwongozo huo na kisha utoe maoni yako kwa kujibu maswali yote au baadhi yake kwa yale utakayopenda kuyatolea maoni HAPA

Taarifa zaidi kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Nidhamu na Mwenendo

Shirika la Wikimedia Foundation lina mpango wa kuanzisha Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Lengo la mwongozo huo ni kujaribu kuainisha vitu vya msingi vinavyopatikana katika miongozo midogo midogo iliyopo tayari katika kila jamii husika (mfano Jumuiya yetu hii ya wahariri wa Wikipedia ya Kiswahili). Lengo hasa la mwongozo huu ni kutengeneza mazingira ambayo wanawikipedia wote duniani watakuwa na uelewa wa pamoja juu ya vitu vya msingi kuhusu nini kinakubalika na kipi hakikubaliki wakati wa uchangiaji (uhariri) wa Wikipedia na pale wanawikipedia wanapowasiliana kwenye Wikipedia au ana kwa ana katika warsha na mikutano ya Wanawikipedia. Wazo hilo limekuja baada kukithiri kwa baadhi ya Wanawikimedia kukumbana kufanyiwa unyanyasaji wa kitabia (mfano matusi, kuitana majina yasiyofaa, kutishiana n.k) na Wanawikimedia wenzao, hivyo kuwakatisha tamaa ya kuendelea kuchangia katika miradi ya Wikimedia.Hivyo, wewe kama mdau muhimu katika miradi ya Wikimedia Foundation, unakaribishwa ku soma zaidi kuhusu mwongozo huo Hapana baada ya kuusoma mwongozo huo unaweza ku toa maoni yako Hapa kabla ya tar 15 April 2020.

Mwaliko wa kujiunga na kundi la Wahariri wa Wikipedia

Nakukaribisha ujiunge na kundi la Wahariri wa Wikipedia kutoka Dar es Salaam ili tuweze kujadiliana na kubadilishana uzoefu na mambo kadha wa kadha kuhusu Uhariri wa Wikipedia. Iwapo utapenda kujiunga, usisite kuwasiliana nasi kupitia wikitzagroup@gmail.com, na kwa taarifa zaidi kuhusu kundi la Wahariri wa Wikipedia wa hapa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla na miradi waliyoitekeleza tayari, unaweza tembelea hapa ukurasa wao wa meta uitwao Wikimedia Community User Group Tanzania au pia katika Facebook kwa jila la Wikimedia Tanzania.

Ndimi AMtavangu (WMF) (majadiliano) 17:44, 5 Aprili 2020 (UTC)Reply

Makala za lugha hariri

Hongera kwa juhudi zako! Mradi unapenda mambo ya lugha, angalia kazi niliyofanya leo ya kurekebisha majina ya lugha nyingi yaliyokosewa upande wa ngeli: Ki- ya badala ya Ki- cha. Karibu kurasa zote nimehamisha juu makala. Sasa naomba wewe urekebishe makala yenyewe kulingana na kichwa kipya. Ukikuta k.mf. Kiswahili ya kisasa, weka Kiswahili cha kisasa. Asante na amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:39, 22 Aprili 2020 (UTC)Reply


Kupanusha makala za Tanzania hariri

Idd Habari zako, naona siku hizi unakazia makumbusho, asante sana. Ilhali unapenda kuchangia na unachapa kazi, nina pendekezo: isingekuwa vibaya kupanusha makala zetu kuhusu Tanzania na Kenya, yaani nchi ambako wasomaji wetu wengi wanaishi. Labda uangalie en:Category:Tanzania. Hapa kuna makala mengi ambayo yanafaa kupelekwa swwiki. Kwa kawaida inasaidia kuanza na jamii ndogo (subcategory) fulani. Maana insaidia kuzoea msamiati wa pekee unaorudiwa, mfano ukianza na en:Category:Economy of Tanzania. Faida yake ni mara nyingi makala hizi zina marejeo tayari. Tahadhari ni: mara nyingi makala si za kisasa, (mfano: kama mkurugenzi wa kampuni anatajwa, au mwanasiasa anatajwa ni waziri, kumbe siyo tena au ameshakufa...), hapa inafaa kuchungulia haraka ka google na kuhakikisha kama ni bado.

Unaonaje? 197.250.228.130 07:35, 6 Mei 2020 (UTC)Reply

Uteuzi kuwa mkabidhi hariri

Salaam! Ulipendekezwa na kukubaliwa kupata haki za mkabidhi. Je, uko tayari kupokea uteuzi huu na kushiriki katika kazi mara kwa mara kama jinsi ilivyoelezwa katika ukurasa wa wakabidhi? Tunaomba jibu lako kwa baruapepe katika wiki hii. Tumia zana za Wikipedia kutuma barua pepe. --'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 07:44, 13 Septemba 2020 (UTC) Reply

We sent you an e-mail hariri

Hello Idd ninga,

Really sorry for the inconvenience. This is a gentle note to request that you check your email. We sent you a message titled "The Community Insights survey is coming!". If you have questions, email surveys@wikimedia.org.

You can see my explanation here.

MediaWiki message delivery (majadiliano) 18:54, 25 Septemba 2020 (UTC)Reply

Kukaribisha wahariri wapya hariri

Ndugu, unapokaribisha mtu, andika "karibu" kwenye ukurasa wake wa mawasiliano, si katika ule wa mtumiaji. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:14, 3 Novemba 2020 (UTC)Reply

Habari Idd, nmekuachia ujumbe katika barua pepe. Czeus25 Masele (majadiliano) 14:20, 8 Desemba 2020 (UTC)Reply

Tuzo ya Uhariri hariri

 

Ninakukabidhi Tuzo ya Uhariri ya Wikipedia kwa juhudi zako za kupitilia kurasa, kukaribisha wageni na kuanzisha makala mapya!

Kipala (majadiliano) 18:06, 7 Desemba 2020 (UTC)Reply

Hongera kwako Idd

Czeus25 Masele (majadiliano) 14:24, 8 Desemba 2020 (UTC)Reply

Ngome Kongwe hariri

Idd habari, nimeona makala ya Ngome Kongwe, nimeipenda. (Isipokuwa " densi za moja kwa moja" - ni ugonjwa wa aina gani? Umetumia ContenTranslation? Ninaitumia pia lakini lazima kuwa macho sana. Wanachomaanisha ni tamasha za ngoma na muziki kwa watalii. - Nimeona picha kwa bahati mbaya ilikuwa giza kidogo. Angalia ukurasa huo: https://sw.wikipedia.org/wiki/Mtumiaji:Kipala/00Test_picha - nimeweka picha uliyotumia na nakala iliyoongezwa mwangaza kidogo kandokando. Si vigumu kuboresha picha kidogo (mimi si hodari), je unayo programu ya picha? Kipala (majadiliano) 15:43, 14 Machi 2021 (UTC)Reply

Habari ndugu Kipala
Nimeweza kuipitia picha na kuitazama, ndio inaonekana kuwa imeongezwa mwanga kidogo ila kwa bahati mbaya kwa sasa sina programu ya picha
Najaribu kuipitia makala hiyo mara kwa mara kuitazama zaidi.
Asante sana Idd ninga (majadiliano) 13:22, 15 Machi 2021 (UTC)Reply
Kuna programu kubwa ambayo ni opensoftware, haina gharama ambayo ni GIMP. Ukiwa na nafasi kwenye laptop, unaweza kuipakua. https://www.gimp.org/, pamoja na https://docs.gimp.org/ (mwongozo) na ukijihusisha nayo sana pia https://wiki.gimp.org/wiki/Main_Page. Kwa kuongeza mwangaza natumia menyu ya Colors >bringhtness/contrast. Kipala (majadiliano) 10:37, 22 Machi 2021 (UTC)Reply
Asante sana
Nimefanikiwa kuipakua Idd ninga (majadiliano) 21:26, 30 Machi 2021 (UTC)Reply

Hongera hariri

Napenda kukupongeza kwa maendeleo yako katika Wikipedia. Endelea kuangalia kama pengine ninarekebisha michango yako ili uzidi kukomaa. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:25, 16 Aprili 2021 (UTC)Reply

Asante sana, nitaendelea kutazama ili nizidi kufahamu zaidi, shukrani sana Idd ninga (majadiliano) 12:00, 16 Aprili 2021 (UTC)Reply
Kwa kweli naona unafuatilia masahihisho na kujifunza vizuri. Pia nakupongeza kwa juhudi za kueneza Wiki yetu. Michango ni mingi, kiasi kwamba sitaweza tena kuipitia yote, hasa ukizingatia kwamba watumiaji wapya wanafanya makosa mengi. Tena kwa kutumia tafsiri ya kompyuta wanatunga kurasa ndefu. Kazi hiyo nakuachieni nyinyi vijana... Ndiyo sababu tuliwachagua kuwa wakabidhi wenzetu! Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:40, 29 Mei 2021 (UTC)Reply
Amani kwako pia.
Tunaendelea kujitahidi zaidi Idd ninga (majadiliano) 07:25, 30 Mei 2021 (UTC)Reply
Kijana Ninga, si fahari sana kufanya tafsiri za kompyuta. Mujitahidi kutumia akili zenu. Si kazi kubwa kama ukijizoeza!--Muddyb Mwanaharakati Longa 08:26, 30 Mei 2021 (UTC)Reply
Sawa kabisa.
Tunaendelea kujitahidi hayo yasitokee tena Idd ninga (majadiliano) 08:38, 30 Mei 2021 (UTC)Reply

Kigezo tafsiri ya kompyuta katika makala ya Ponta de Vera Cruz hariri

Habari Idd ninga, hongera sana katika jitihada za kupitia makala nyingi na kuzirekebisha. Nimeona kwenye makala ya Ponta de Vera Cruz umeweka kigezo cha tafsiri ya kompyuta ni sawa kabisa ila makala ile ni fupi sana kiasi kwamba naona ingekua bora zaidi kama ungerekebisha makala ile iweze kueleweka vizuri. Nahisi kwa kufanya hivyo makala hiyo ingekua bora zaidi. Amani kwako! --CaliBen (majadiliano) 07:20, 6 Juni 2021 (UTC)Reply

Asante
Naifanyia marekebisho zaidi Idd ninga (majadiliano) 07:35, 6 Juni 2021 (UTC)Reply

Can you help me correct an article? Thank you! hariri

Hello, @Idd ninga:! I wrote an article on Andrea Benetti, a well-known Italian artist https://en.wikipedia.org/wiki/Andrea_Benetti_(artist). I used the automatic translator to make a draft https://sw.wikipedia.org/wiki/Mtumiaji:BarbaraLuciano13 . Could you help me correct the text and add the infobox with the photo at the beginning and the categories at the bottom? Unfortunately I don't know the language and I am not able to do it ... Thanks for what you can do, see you soon, --BarbaraLuciano13 (majadiliano) 09:12, 19 Juni 2021 (UTC)Reply

Hello,
No problem i will do it soon Idd ninga (majadiliano) 09:15, 19 Juni 2021 (UTC)Reply

Kuhamisha ukurasa wa mtumiaji hariri

Ndugu Idd, usihamishe ukurasa wa mtumiaji kwenda majadiliano. Kama Aneth alikosea kuweka karibu katika ukurasa wa mtumiaji, hukutakiwa kuhamisha. Ulitakiwa ufungue msimbo, ondoa katika ukurasa wa mtumiaji na uyaweke katika majadiliano. Kitendo cha kuhamisha maana yake umefuta ukurasa wa mtumiaji huyo!--Muddyb Mwanaharakati Longa 09:38, 28 Juni 2021 (UTC) Reply

Shukrani sana, hata mimi baada ya kufanya hivyo nikaona kuna jambo halijakaa sawa, nashukuru kwa maelekezo mazuri Idd ninga (majadiliano) 09:51, 28 Juni 2021 (UTC)Reply
Pamoja sana, mkuu! Jambo limeisha hilo!--Muddyb Mwanaharakati Longa 09:55, 28 Juni 2021 (UTC)Reply
Safari hii umefanya vizuri. Usiwe na shaka! Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 03:36, 1 Agosti 2021 (UTC)Reply

Sahihi na tarehe hariri

Idd, habari? Naona mara kadhaa jina lako chini ya mchango lakini bila tarehe. Sijui kama ni setting fulani? Au unaingiza jina lako mwenyewe? Je unatumia alama ya ~~~~  ? Kipala (majadiliano) 12:00, 23 Agosti 2021 (UTC)Reply

Salamu, nilichelewa kukujibu kwa siku kama tatu hivi sikuingia vizuri humu,naona inatokea hivyo kwa sababu siweki hiyo alama,ila ngoja niijaribu,Idd ninga (majadiliano) 21:46, 24 Agosti 2021 (UTC)Reply
Naona imekaa sawa sasa, Idd ninga (majadiliano) 21:46, 24 Agosti 2021 (UTC)Reply
Safi sasa! Kipala (majadiliano) 22:48, 24 Agosti 2021 (UTC)Reply

Tafsiri kompyuta hariri

Habari naona ulimwonya mtumiaji:Awadhi_Awampo bila kuchukua hatua zaidi. Nimemzuia sasa. SIjui sababu zako za kumwonya tu zilikuwaje (si lazima kuniambia, ninaheshimu azimio lako), ila kuna njia nyepesi kuona kama hapa ni mfano wa kukosa lugha au uwivu wa kutumia tafsiri ya google. Ulitambua Kiswahili chake hakieleweki. Nikiona hayo mimi, namwaga matini ya enwiki kwenye translate.google.com na kulinganisha. Nikiona mifano zaidi ya mbili amenakili 1:1 pia kuna ugumu wa kuelewa, ninamzuia. Uzembe huu wa kumwaga google-translate bila kujali matokeo ni ugonjwa mbaya. Heri tutibu. Kipala (majadiliano)

Hassan bin Omari hariri

Niliandika makala hii mimi mwenyewe katika Kiingereza, na tafsiri pia nimefanya mwenyewe, bila kufuata Google translate. Sijui kwa nini umeona dalili za komputa humo. Ingewezekana kuboresha Kiswahili kile, na mimi ninayo uwezo zaidi katika vilugha vyingine, ningeshukuru msaada wowote. Pia, nimepakia faili ya "Sha'iri la Makunganya" katika wikisource - https://wikisource.org/wiki/Sha%27iri_la_Makunganya - na mimi sina ujuzi wa kufanya kiungo kile cha'wikisource' katika makala ya Hassan bin Omari, ili watu wangependa waweza kusoma shairi lile. Asante.


Africa Wiki Challenge 2021 hariri

Dear Idd in (Idd in), Congratulations for winning this year's Africa Wiki Challenge. You are by this mail invited to join our 2021 Annual General Meeting and Award Ceremony on:

Date: 2nd December 2021 Time: 10:00 AM to 13:00 PM UTC via zoom. Links on our streaming will be made available to you in our next email. While waiting, is there any shop that allows online purchase to be made? Regards, Christabel - Naa Tsotsoo Naa Tsotsoo (Naa Tsotsoo)(talk) [reply]

How we will see unregistered users hariri

Hi!

You get this message because you are an admin on a Wikimedia wiki.

When someone edits a Wikimedia wiki without being logged in today, we show their IP address. As you may already know, we will not be able to do this in the future. This is a decision by the Wikimedia Foundation Legal department, because norms and regulations for privacy online have changed.

Instead of the IP we will show a masked identity. You as an admin will still be able to access the IP. There will also be a new user right for those who need to see the full IPs of unregistered users to fight vandalism, harassment and spam without being admins. Patrollers will also see part of the IP even without this user right. We are also working on better tools to help.

If you have not seen it before, you can read more on Meta. If you want to make sure you don’t miss technical changes on the Wikimedia wikis, you can subscribe to the weekly technical newsletter.

We have two suggested ways this identity could work. We would appreciate your feedback on which way you think would work best for you and your wiki, now and in the future. You can let us know on the talk page. You can write in your language. The suggestions were posted in October and we will decide after 17 January.

Thank you. /Johan (WMF)

18:19, 4 Januari 2022 (UTC)

Kituo cha reli Diez Ost hariri

Hello Bro,

you re fluent in Kiswahili language, I live close to the town Diez where this station is located in, do you want to finish up this article together? 84.143.56.111 16:54, 9 Januari 2022 (UTC)Reply

Alex

Have you voted in the UCoC enforcement guidelines ratification? hariri

Hi! @Idd ninga:

The ratification voting process for the revised enforcement guidelines of the Universal Code of Conduct (UCoC) is now open! Voting commenced on SecurePoll on 7 March 2022 and will conclude on 21 March 2022. Please read more on the voter information and eligibility details.

Please vote and encourage other editors of Swahili Wikipedia to also vote.

Regards, Zuz (WMF) (majadiliano) 12:22, 11 Machi 2022 (UTC)Reply

Spam hariri

Hello @Idd ninga, I hope you're doing well. Please delete the spam article Nasir Chaudhry. For more information have a look here. Thanks for your consideration. C1K98V (💬 ✒️ 📂) 14:27, 6 Desemba 2022 (UTC)Reply

Hello, i am going to do it, Peace Idd ninga (majadiliano) 07:22, 8 Desemba 2022 (UTC)Reply

Sensa hariri

Ndugu, nimerudisha kurasa ulizosasisha kwa sababu umeweka idadi ya watu wa mkoa mzima kama idadi ya wakazi wa mji wa Arusha tu. Pole na amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:19, 20 Desemba 2022 (UTC)Reply

Asante sana, naona ni error kidogo,nilikusudia mkoa wa Arusha,Asante kwa Masahihisho hayo, Amani sana Idd ninga (majadiliano) 13:20, 20 Desemba 2022 (UTC)Reply

Pendekezo la Ufutaji hariri

Salaam Idd ninga,

Pongezi kwa majukumu, samahani naomba pitia makala hii Wanawake Watetezi Wa Haki za Binadamu na hii hapa Wanawake watetezi wa haki za Binadamu ni makala moja iliyoanzishwa mara mbili ikiwa na utofauti wa herufi za mwanzo wa neno (kubwa na ndogo), hivo wewe kama mkabidhi naomba saidia kupitia makala hizo na ufute moja wapo kati ya hizo ili kupunguza mkusanyiko wa makala zenye maudhui sawa.

Ahsante sana, amani kwako Anuary Rajabu (majadiliano) 15:56, 19 Januari 2023 (UTC)Reply

Asante sana, nazitazama sasa ,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 16:10, 19 Januari 2023 (UTC)Reply
Ahsante sana kwa kuzingatia Anuary Rajabu (majadiliano) 16:12, 19 Januari 2023 (UTC)Reply

Msaada hariri

Salaam Idd ninga,

Samahani, pengine upo na majukumu mengi muda huu naomba nisaidie kufuta ukurasa huu kwani nimeunzisha kwa makosa.

Asante Anuary Rajabu (majadiliano) 08:31, 30 Januari 2023 (UTC)Reply

Kitendo kimekwisha,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 08:51, 30 Januari 2023 (UTC)Reply
Asante sana, sote tuendelee kuijenga Wikipedia ya Kiswahili Anuary Rajabu (majadiliano) 12:57, 30 Januari 2023 (UTC)Reply