Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Anuary Rajabu (majadiliano) 13:55, 6 Mei 2023 (UTC)Reply

Ndugu, umebadilisha kabisa makala juu ya ushoga ilingane na mtazamo usiolingana na ule wa kawaida wa wasemaji wa lugha ya Kiswahili, tena wakati tulikuwa bado tunajadiliana juu ya hilo. Huu si utaratibu wa Wikipedia. Imenibidi kurejesha ukurasa wa awali. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:02, 3 Septemba 2023 (UTC)Reply

Ndugu Riccardo Riccioni,
Nakushukuru kwa kushiriki katika majadiliano haya. Ni muhimu kutambua kuwa Wikipedia inalenga kuwa chanzo cha taarifa zenye msingi wa ushahidi na elimu kwa umma. Wakati wa kuhariri makala kuhusu masuala ya utambulisho wa kijinsia na mapenzi ya jinsia moja, ni muhimu kuzingatia miongozo ya Wikipedia na kutumia sayansi na ushahidi kutoa habari sahihi.
Majadiliano na maelezo yanayotolewa katika makala yana nafasi katika Wikipedia, na mchango wa wanachama kama wewe ni muhimu katika kuboresha uelewa wa umma. Hata hivyo, inaweza kuwa muhimu kufanya majadiliano ya kina na kufikia maridhiano katika suala hili ili kuhakikisha kwamba taarifa zinazotolewa zinakidhi viwango vya Wikipedia na heshima kwa maoni ya watumiaji wote.
Tutie bidii kuhakikisha kuwa mjadala huu unazingatia miongozo na viwango vya Wikipedia na unafanyika kwa heshima na kufungua fursa ya kuboresha uelewa wa umma kuhusu masuala haya muhimu. Amani kwako pia! CuriousScientist1 (majadiliano) 08:16, 3 Septemba 2023 (UTC)Reply
Ndugu, imenipasa kukuzuia kwa siku 3 kwa sababu unalazimisha katika Wikipedia ya Kiswahili tukubali hoja zako ambazo labda zinatetewa na Wikipedia ya Kiingereza, lakini si za kisayansi tu kama unavyosema wewe. Kuna mengine mengi nyuma yake. Nionavyo mimi, viwango vya Wikipedia havifuatwi katika lugha hiyo kwa sababu mchango wowote tofauti unazuiwa, kinyume cha neutrality iliyotarajiwa. Wewe unajifanya refa wa mechi wakati ni mchezaji mmojawapo, tena wa dharura: mbona hujawahi kuchangia mada nyingine yoyote kwetu? Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:28, 3 Septemba 2023 (UTC)Reply
Ndugu Riccardo Riccioni,
Ninaelewa kwamba kuna tofauti katika maoni yetu kuhusu marekebisho katika Wikipedia ya Kiswahili. Kama mwenzako katika jamii ya Wikipedia, natambua umuhimu wa majadiliano na kuheshimu maoni ya wengine.
Ninakubaliana nawe kwamba viwango vya Wikipedia vinapaswa kufuatwa katika lugha zote, pamoja na Kiswahili. Majadiliano na kurekebisha makala ni sehemu ya mchakato wa kuboresha taarifa za Wikipedia. Kila marekebisho yanapaswa kuwa na msingi wa vyanzo vinavyoaminika na taarifa zenye ushahidi wa kisayansi na ukweli.
Nimejitolea kuchangia katika maeneo ambayo nina maarifa na uelewa, na nitajitahidi kuheshimu viwango vya Wikipedia na kanuni za jamii. Naamini kwamba majadiliano yenye heshima na kutoa taarifa zenye ushahidi zitatusaidia kufikia muafaka na kuboresha taarifa za Wikipedia kwa manufaa ya watumiaji wote.
Amani kwako pia, na natumai tutaweza kufanya kazi kwa pamoja kujenga jukwaa la elimu na taarifa bora katika lugha ya Kiswahili. CuriousScientist1 (majadiliano) 11:33, 3 Septemba 2023 (UTC)Reply