Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Twamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo - hata kuitafsiri kutoka katika Wikipedia kwa lugha nyingine. Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wa sanduku la mchanga. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike pekee kwenye ukurasa wako wa mtumiaji baada ya kufungua akaunti. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho. Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje
  • wala matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, MediaWiki Content Translation, etc.)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:30, 19 Desemba 2020 (UTC)

Kuhusu UhaririEdit

Habari ndugu Anuary Rajabu Hongera sana kwa jitihada zako za kuhariri katika Wikipedia ya Kiswahili, jaribu kupitia sana ukurasa wa mabadiliko ya karibuni ili kuweza kuona baadhi ya makala zako na namna zinavyoendelea kuboreshwa, na utumie maboresho hayo katika makala zako nyingine. Amani sana kwako. Idd ningaIdd ninga (majadiliano) 22:58, 23 Mei 2021 (UTC)

VolkenoEdit

Ndugu naona tunaingiliana kwenye makala kuhusu Chamko ya volkeno. Sijamaliza bado. Ushauri ni: uangalie historia ya makala; kama imehaririwa dakika chache zilizopita, kuna uwezekano mhariri bado anaendelea.. Kwa hiyo heri kusibiri hadi kesho. Kipala (majadiliano) 20:05, 25 Mei 2021 (UTC)

Ooh Sawa kiongozi nimekuelwa Samahani kwa hilo, Nitafanya hivo. Anuary Rajabu (majadiliano) 22:17, 25 Mei 2021 (UTC)

Jina la MtuEdit

Salamu Anuary Rajabu Unaweza kuangalia katika makala zako zenye majina ya watu na kuona baadhi ya mabadiliko hasa ya masahihisho ya jina, kwa kawaida unapoandika jina la mtu inafaa kabisa jina liandikwe kwa herufi kubwa badala ya ndogo, unaweza kuona namna majina ya makala zako yalivyobadilishwa, hongera kwa juhudi unazofanya, endelea kujifunza zaidi, Idd ninga (majadiliano)

Nimekuzuia siku 3Edit

Ndugu, uliondoa vigezo vya umaarufu, vyanz na futa kutoka ukurasa wa Melody Mbassa, bila maelezo yoyote. Hapa umeingilia katika kazi ya usimamizi wa wikipedia hii. Nimekuzuia sasa kwa siku 3, huwezi kuhariri kwa siku hizo. Unaweza kujieleza kwenye ukurasa huu hapa. Ukiweza kutaja sababu zinazoeleweka naweza kuondoa kizuizi.Kipala (majadiliano) 08:41, 28 Mei 2021 (UTC)

Naomba kusamehewa,nilikua sijui kuhusu hilo lakini kwa kuwa kiongozi wangu ameweza kunielekeza kuhusu hilo, sitoweza kufanya hivo tena kwani mie sio mjuzi sana katika uhariri wa makala. Hivo nimeweza kujifunza. Anuary Rajabu (majadiliano) 09:07, 28 Mei 2021 (UTC)

Asante kwa kujibu. Nimekufungua. Ila bado hujasema kwa nini uliondoa vigezo vile? Kipala (majadiliano) 18:57, 28 Mei 2021 (UTC)

Can you help me correct an article? Thank you!Edit

Hello, @Anuary Rajabu:! I wrote an article on Andrea Benetti, a well-known Italian artist https://en.wikipedia.org/wiki/Andrea_Benetti_(artist). I used the automatic translator to make a draft https://sw.wikipedia.org/wiki/Mtumiaji:BarbaraLuciano13 . Could you help me correct the text and add the infobox with the photo at the beginning and the categories at the bottom? Unfortunately I don't know the language and I am not able to do it ... Thanks for what you can do, see you soon, --BarbaraLuciano13 (majadiliano) 09:11, 19 Juni 2021 (UTC)

MarekebishoEdit

Salamu Anuary, tazama katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Entisar_Elsaeed kuna sehemu umeandika kuwa Entisari ni mwanaharakati wa kutetea Wanawake, lakini katika makala hii ukasema kuwa Elsaeed na taasisi yake walilenga katika kuongeza unyanyasaji wa wanawake majumbani, nafikiri kuwa ulitaka kuandika kupunguza, sasa cha kufanya pitia makala yake ni kuifanyia marekebishom, tazama katika makala ya kiingereza nini kilichoandikwa,Amani sanaIdd ninga (majadiliano) 18:34, 9 Machi 2022 (UTC)

sawa kiongozi nimeelewa nitafanya hivyo. Anuary Rajabu (majadiliano) 12:47, 10 Machi 2022 (UTC)

HongeraEdit

Anuary naona siku hizi unaleta michango mingi yenye thamani. Naona umeshika vizuri fomati ya wikipedia. Nakupa Hongera! Kipala (majadiliano) 07:59, 16 Machi 2022 (UTC)

Asante sana. Anuary Rajabu (majadiliano) 11:34, 16 Machi 2022 (UTC)
Pamoja na pongezi, naomba uangalie makala zenyewe: kweli tunahitaji kutetea ushoga? Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:13, 29 Machi 2022 (UTC)
Asante kwa kufanyia doria makala nyingi. Mimi nimezidiwa. Ila naomba uondoe tanbihi za Wikipedia ya Kiingereza na hasa jamii nyingi mno. Unakuta makala ya mwanamuziki wa Nigeria ina jamii:Sanaa ya Afrika! kama si Jamii:Afrika! Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:14, 4 Mei 2022 (UTC)
Asante sana, nitajitahidi kufanya hivyo. Amani iwe nasi sote. Anuary Rajabu (majadiliano) 14:31, 4 Mei 2022 (UTC)

JAMII za Muziki Aziingiliani na michezoEdit

Amani kwako ndugu, kuwa makini wakati unachagua jamii ya kuweka kwenye makala,acha kuunganisha jamii ya muziki na makala za mchezo wa Mpira wa miguu. Justine Msechu (majadiliano) 19:41, 14 Mei 2022 (UTC)

Asante kwa ukumbusho nadhani ni suala la kujisahau tu katika ukopiji wa jamii wakati wa kuchapisha makala, hivo nitazipitia makala zangu zote ili kurekebisha makosa hayo. Amani iwe nasi sote. Anuary Rajabu (majadiliano) 19:54, 14 Mei 2022 (UTC)

Feminism and Folklore 2022 - Local prize winnersEdit

Please help translate to your language

Congratulations for winning a local prize in Feminism and Folklore 2022 writing competition. Thank you for your contribution and documenting your local folk culture on Wikipedia. Please fill in your preferences before 15th of June 2022 to receive your prize. Requesting you to fill this form before the deadline to avoid disappointments.

Feel free to contact us if you need any assistance or further queries.

Best wishes,

FNF 2022 International Team

Stay connected     

MediaWiki message delivery (majadiliano) 07:50, 22 Mei 2022 (UTC)

Reminder to provide information - Feminism and Folklore 2022Edit

Dear User

The Google form to submit information of winners during the 2022 edition of Feminism and Folklore 2022 end on 10th of June 2022. Please be informed that you will loose your prize once the deadline for sending information ends. We humbly urge you to kindly fill the form using this link as soon as possible.

Feel free to contact us on mail or talkpage if you have any difficulties.

Thank you for understanding!

Regards

International Team

Feminism and Folklore 2022

MediaWiki message delivery (majadiliano) 12:38, 5 Juni 2022 (UTC)

Mipira ya samakiEdit

Salamu Anuary. Ukichangia makala unafuata mabadiliko katika makala haya na kusoma majadiliano yake? Niliweka maoni yangu na swali kwenye Majadiliano:Mipira ya samaki (angalia hapo chini). Bado ninangoja jibu lako.

Mipira wa samaki ni tafsiri isiyofaa kwa "fish balls". Maana ya mpira kwanza ni "rubber", kwa hivyo ikiwa maana yake ni "ball" hiyo ball ni aina ya rubber au labda ya plastiki. Kwa ujumla, "food ball" ni tonge kwa Kiswahili, au kitonge ikiwa ni dogo. "Meat ball" ni kababu, kwa hivyo labda tutumie hii kwa "fish ball" pia. Mnapendelea neno gani? ChriKo (majadiliano) 06:00, 22 Juni 2022 (UTC)

Asante sana Chriko kwa ukumbusho wako mzuri, hakika kweli Mipira ya samaki sio tafsiri thabiti ya "fish ball", hivyo katika kuchangia kwangu uhariri wa makala hiyo sikuweza kupitia huo ujumbe wako ulioacha. Anuary Rajabu (majadiliano) 02:16, 23 Juni 2022 (UTC)