Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Mr Accountable (majadiliano) 15:04, 24 Novemba 2009 (UTC)Reply

Makala ya Bidco hariri

Salam, Njenga. Eti, unaweza kuongeza kitu kama INTERWIKI kwenda Wikipedia nyingine? Makala hiyo haina viungo vya INTERWIKI - au umetunga mwenyewe kwa kufuata marejeo ya kampuni?--MwanaharakatiLonga 11:44, 31 Desemba 2009 (UTC) Reply

Salaam! Haya, fanya mpango wa kutafsiri vigezo vile. Haitakiwi vigezo viwe kwa Kiingereza - kwani itakuwa haileti maana. Tafadhali anza kutafsiri vigezo vile.--MwanaharakatiLonga 10:30, 7 Januari 2010 (UTC)Reply
Haya, fanya mpango tuwasiliane hapa.--MwanaharakatiLonga 11:39, 7 Januari 2010 (UTC)Reply
Erick, umepiga hatua. Ninafurahi kuona kwamba si mwoga wa kujaribu. Kile kigezo cha michuano ya golf kimekaa bomba ile mbaya. Umefaulu, kaka. Halafu? Nimeona mara nyingi una-wasilisha mjadala wako bila kutia sahihi yako. Yaani, kama jinsi unavyoona kwangu miye - mwishoni linakuja jina na tarehe ya mjadali liofanyika. Ukitaka kuweka sahihi yako, tafadhali andika alama hizi --~~~~ mwishoni kabisa mwa maelezo yako! Kila la kheri halafu pitia tena ule mjadala wa awali kuhusu MALL!--MwanaharakatiLonga 12:30, 7 Januari 2010 (UTC)Reply

Tuzo hariri

Salam, Erick. Eti, kuna zawadi ziligawiwa? Ikiwa kuna zawadi, basi watu wa google ndiyo wanajua na si sisi watu Wikipedia. Mengi wanafanya wenyewe kivyao-vyao na wala hawatuambii lolote kuhusu zawadi. Pole! Je, umepokea tuzo au zote zitatolewa mpaka hapo mwisho wa siku?--MwanaharakatiLonga 14:25, 14 Januari 2010 (UTC) Reply

Kuna watu walishinda na wakaziendea zawadi zao katika ofisi za Google huku Kenya. Kile ambacho ningependa kujua ni, wale wa Tanzania watapataje zawadi zao?? --Erick njenga (majadiliano) 14:51, 14 Januari 2010 (UTC)Reply
Aah, basi hii ishakuwa utata! Kumbe, kuna wengine wamepata (hasa hao wa Kenya), hawa wa Bongo (bado kitendawili). Sijui itakuwaje. Labda mwisho wa siku watazileta kwa pamoja! Je, kuna yeyote unayemjua huko mjini Nairobi ambaye alipata kushinda? Na kama yupo, basi mwulize wapi pa kuweza kupata zawadi kwa wale washindi wa Dar es Salaam. Cheers.--MwanaharakatiLonga 15:01, 14 Januari 2010 (UTC)Reply
Nilimuuliza akaniambia hajui pale ofisi za google zipo huko dar. Lakini nadhani kuwa punde shindano litakapoisha, watapeana zawadi zote kwa ujumla. Asante!--Erick njenga (majadiliano) 15:04, 14 Januari 2010 (UTC)Reply

Ingvar Kamprad hariri

Uliandika kuhusu Ingvar Kamprad, sindiyo? Uliandika Kamprad atoke "Uswisi" lakini anatoka USWIDI. Nchi hizi zipo tofauti kabisa. Uswidi ni ukubwa zaidi na waswidi wanasema Kiswidi lakini waswisi wanasema Kiitalia, Kifaransa, Kijerumani na lugha moja nyingine.

Nyayo Cars hariri

Hi, I want to use the File Nyayo Cars.JPG in the German Wikipedia. Would be nice if you could move this file to the Wikimedia Commons. --TheAutoJunkie (majadiliano) 03:50, 12 Aprili 2010 (UTC)Reply