Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Baba Tabita (majadiliano) 07:09, 26 Julai 2011 (UTC)Reply

Kingala au Kilingala?

hariri

Bwana Kwamikagami, salaam. Nimeona umebadilisha viungo vyote vya Kilingala kuwa Kingala. Bahati mbaya, siwezi kupata jina hilo mtandaoni. Ukigoogle "Kingala" ni jina la kijiji au la mtu lakini ukigoogle "Kilingala" utapata lugha. Linganisha http://www.google.co.ke/search?q=Kingala+kwenye&ie=utf-8&oe=utf-8&aq=t&rls=org.mozilla:en-US:official&client=firefox-a na http://www.google.co.ke/search?q=Kilingala+kwenye&ie=utf-8&oe=utf-8&aq=t&rls=org.mozilla:en-US:official&client=firefox-a Naomba utafakari na kurudisha hali ya Kilingala. Asante. --Baba Tabita (majadiliano) 18:08, 14 Desemba 2011 (UTC)Reply

Inaonekana wewe ni sahihi, bwana. Ni kama kusema "Kikiswahili", lakini lugha ni ambayo watu kusema. Kwamikagami (majadiliano) 22:36, 14 Desemba 2011 (UTC)Reply
Wakati mwingine usikurupuke kubadilisha vitu bila kufanya utafiti!--MwanaharakatiLonga 06:03, 15 Desemba 2011 (UTC)Reply

Ndoa za jinsia moja

hariri

Ndugu, kama ulivyoelekezwa hapo juu, usifanye mabadiliko kwa kujiamini mno, hasa ukitaka kurekebisha yaliyoandikwa na wakabidhi wa Wikipedia yetu. Tumefanya kazi miaka mingi kwa maelewano, hivyo usifikiri wote hawaelewi mambo. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:07, 25 Julai 2019 (UTC)Reply

Alama za nyota

hariri

Ndugu umefanya kazi kubwa kuingiza alama hizo zote katika makala ya Makundinyota 88 ya UKIA. Utaona nimerudisha hali ya awali. Sababu yangu ni: hujaeleza kama alama hizo zimekubaliwa na wataalamu, kwa mfano UKIA. Alama hizi umezipata wapi? Chanzo? Je kuna haki za picha hizo? Sikatai kurudisha kama una majibu ya maswali. Kipala (majadiliano) 20:56, 5 Oktoba 2021 (UTC)Reply

Nisipokosei chanzo kiko hapa https://www.suberic.net/~dmm/astro/constellations.html. Je una ushahidi wowote kwamba alama hizo zimekubaliwa au kutumiwa na mtu yeyote mbali na mchoraji aliyezitunga?Kipala (majadiliano) 21:17, 5 Oktoba 2021 (UTC)Reply

Habari ndugu,

Hakuna haki za picha hizo. Sio rasmi, zimependekezwa tu. Zinatumika katika:

Peter Grego (2012) The Star Book: Stargazing Throughout the Seasons in the Northern Hemisphere. F+W Media.

F+W Media (1913–2019) ilikuwa mchapishaji wa gazeti la Sky & Telescope. F+W sasa ni sehemu ya Penguin Books / Random House.

NASA imetumia alama zingine zilizoundwa na Moskowitz, haswa zile za Eris, Makemake na Haumea ( ,  ,  ). Za Eris na alama zake za Sedna ( ) iko kwenye Unicode.

Kwamikagami (majadiliano) 23:03, 5 Oktoba 2021 (UTC)Reply