Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Kipala (majadiliano) 09:39, 27 Novemba 2021 (UTC)Reply

Asante kwa makala zako, ila angalia marekebisho niliyozifanyia, ili usirudie makosa yaleyale. Kwa mfano, madondoo yasitaje Wikipedia ya Kiingereza. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:51, 1 Desemba 2021 (UTC)Reply
SAWA Mimi Prowess (majadiliano) 15:10, 1 Desemba 2021 (UTC)Reply
Mbona umerudia makosa yaleyale? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:00, 10 Februari 2022 (UTC)Reply
hello Mimi Prowess (majadiliano) 11:36, 5 Agosti 2022 (UTC)Reply
Bado sijajua nn shida naomba uni unblock Mimi Prowess (majadiliano) 13:09, 4 Oktoba 2022 (UTC)Reply

Nimekuzuia wa sababu niemona tena makala kutoka mkono wako ambazo hazieleweki halafu zinasababisha kazi nyingi ya kusafisha. Naona unajitahidi kusahihisha tafsiri ya google lakini matokeo hazieleweki, makala hazi hazidsaidii kitu. Ninakuzuia sasa kwa muda naomba uwasiliane nami kwa kufungua ukurasa wangu (bofya jina langu chini) na kuniandikia baruapepe kwa kubofya “Email this user” upande wa kushoto. Hapo nitaweza kukuruhusu tena. Hapo lazima uwezeshe njia kwa kufuata maelezo katika Wikipedia:Email. Kipala (majadiliano) 12:57, 4 Oktoba 2022 (UTC)Reply

Makala zingine ni asili yake kuwa na misamiati migumu . Huwezi kusoma mara moja na kuilewa hivyo rudia vizuri kisha ndo ublock mtu. Hii si sawa kuwa unablock mtu unapohisi ww yeye amekosa . Mimi Prowess (majadiliano) 13:55, 4 Oktoba 2022 (UTC)Reply
Rafiki kwanza aliyekuzuia ni mimi Kipala, si Riccardo aliyewasiliana nawe awali. Sisi sote wawili tuko kati ya wakabidhi waliochaguliwa a wanawikipedia kuangalia utaratibu humo.
Nimekuzuia kwa sababu uliombwa awali kuleta makala safi. Sasa naona Harakati za Wikimedia na Tasnifu za Wikipedia ambayo haieleweki kabisa. Je unajua kwamba tasnifu na "plagiarism" ni mambo tofauti, hata kama moja inaweza kutokea katika nyingine? Sentensi ya kwanza si Kiswahili. Zile zinazofuata vilevile.
Michango ya aina hii inaharibu hadhi ya wikipedia yetu. Pendekezo langu: ninaweza kukuruhusu tena ukiahidi mawili
  1. utaanzisha makala katika nafasi yako ya mtumiaji pekee halafu utamtafuta mwanawikipedia mwenye maarifa (hata Riccardo au mimi) kupitilia yale uliyoandaa
  2. unaweza kupeleka makala katika nafasi ya makala baada ya kupokea jibu la Ndiyo. (kama makala mbili hazikufutwa bado, unaweza kuweka umbo jipya badala yake. Kama zimeshafutwa, unaweza kuanza upya - baada ya kupokea "Ndiyo")
Maelezo jinsi ya kutunga katika nafasi yako ona hapa: Msaada:Jaribio. Tafadhali soma kwanza na uniambie kama umeelewa yote, menginevyo uliza swali. Kipala (majadiliano) 17:06, 4 Oktoba 2022 (UTC)Reply
Sawa naomba email yako Mr Kipala Mimi Prowess (majadiliano) 14:29, 6 Oktoba 2022 (UTC)Reply
Nmeelewa. Mimi Prowess (majadiliano) 12:31, 21 Novemba 2022 (UTC)Reply