Ndugu Side, karibu kwenye wikipedia ya Kiswahili! Kuna kazi nyingi. Naomba uangalie makala ya "Msaada wa kuanzisha makala" (utaipata pia kwa kubonyeza "msaada" hapo upande wa kushoto). Ukiwa na swali lolote uliza tu. --Kipala 13:51, 13 Oktoba 2007 (UTC)Reply

Karibu katika wikipedia ya kiswahil. Unaruhusiwa kuchangia makala jisikie huru wala usihofu tupo pamoja. Unaweza kuapata Msaada wa kuanzisha makala kwa bonyeza hapa --Muddyb Blast Producer 13:41, 18 Oktoba 2007 (UTC)Reply

Kiwalani

hariri

Ndugu Side, nimehariri kidogo makala yako ya Kiwalani. Ukiangalia "historia" utagundua ya kwamba nilisahihisha hasa mambo mawili:

  • kuondoa nafasi mwanzo wa mstari inayosaabisha fremu kutokea na rangi kuwa kijivu-kijivu
  • kuingingiza au kusahihisha viungo kwa mfano kuingiza majina ya makala yaliyopo tayari (airport ile, au mkoa wa Dar). Pia ambayo ni muhimu: Jamii au Category inayosaidia kupatikana kwa makala baadaye.

Ukiona nilifanya kaosa basi rudisha. --Kipala 14:23, 22 Oktoba 2007 (UTC)Reply

Sidemontero

hariri

Ndugu Side, naomba uhamishe yaliyomo ya makala "Sidemontero" kwenda ukurasa wako wa user:sidemontero. User page ni sawa lakini haifai kwa makala. --Kipala 11:39, 29 Oktoba 2007 (UTC)Reply

Umekulupuka

hariri

Salam nyingi Nd. Said, Haya habari za dar natumai husalama wa afya. Nd. said naona umekulupuka kuandika habari zako binafsi kwa njia ya makala, ilhali ipo njia nyingine ya kufanya ili habari zako zieleweke. Ushauri: Inabidi habari zako zote uweke kwenye User page, hapo unaruhusiwa kuweka yote yanayo kuhusu na siyo katika makala. Tafadhali hamisha zile taarifa zako katika makala ya Sidemontero na uhamishie hapa. Ahsante.--Mwanaharakati 12:42, 30 Oktoba 2007 (UTC)Reply

Kaza buti

hariri

Salam nyingi Nd. Said, naona makala zako nyingi tu, zeneye kuhusu masuala ya filamu za waigizaji wa televisheni, inaonekana ni kiasi gani unajali wiki hii ya kiswahili iwe na habari za waigizaji wa katika TV. Si kitu. Unaweza kuandika makala vile upendavyo, kisichotakiwa ni matusi na lugha zisizoeleweka, basi. Kila lakheri--Mwanaharakati 10:51, 3 Novemba 2007 (UTC)Reply

Shaaban Robert

hariri

Salam nyingi Nd. Said. Nimeona habari za Shaaban Robert, kweli kuna makosa yametendeka. Ushauri:

  1. Tutoe taarifa kwa moja ya wakabidhi juu ya hili.
  2. Tumuelezee huyu bwana kwa kirefu kuliko ulivyokuwa mwanzo.

Au we waonaje? haya basi. Mengineyo: Unaonaje jina la mwanaharakati ukijiita B.(Mwanaharakati B. Badala ya mimi) Maana hii italeta mchanganyo kidogo. Sizani kama wakabidhi watatuelewa vizuri. Ni lazima tuweke alama rahisi, ni vyema kila mtu akiweka jina tofauti na la mwenzake ili kurahisha mawasiliano. Ni ushauri tu una hiyari yako kuufuata au la. Haya basi tuendelee na Shaban Robert. --Mwanaharakati 05:32, 13 Novemba 2007 (UTC)Reply

Mnaonaje mkihamisha majadiliano kuhusu Shaaban Robert kwenda ukurasa wa majadiliano huko kwenye makala yenyewe? Mkiwa na uhakika musahihishe tu menginevyo ni kwanza kutaja kwenye ukurasa wa majadiliano kasoro zile zinazoonekana na kusubiri siku moja, mbili.. --Kipala 07:10, 13 Novemba 2007 (UTC)Reply

Karibu tena

hariri

Salam. Naona ulitukimbia kabisa katika wiki hii. Lakini naona ujio huu sio ujio wa Bush ndani ya Iraki au Beckham ndani ya Real Madrid, ama Yesu Kristo katika Nazareth, naona ni ujio wa kipekee!!! Basi karibu sana Nd. Said Montero wa Abdalah katika Kamusi elezo huru ya Kiswahili...--"Mwanaharakati" (talk) 13:22, 29 Februari 2008 (UTC)Reply

Wentworth Miller

hariri

Salam. Natumai utakuwa umeona baadhi ya mabadilisho niliyofanya katika ukurasa wa kichwa cha habari husika hapo juu. Nimebadilsiha namna ya kutaja miaka na tarehe ya kuzaliwa katika sehemu ya mwazoni na kuongeza baadhi ya maelezo yanamhusu Wentworth Miller. Ukiona nimekosea, waweza kurudisha yale maelezo yako ya awali! Karibu sana...--"Mwanaharakati" (talk) 12:55, 5 Machi 2008 (UTC)Reply

Ahsante kwa hilo.--SideMontero (majadiliano) 13:44, 11 Machi 2008 (UTC)Reply

Hoya mwana, nasikia hapo Buguruni ulipo pc zao zina vimeta kinyama. Je hilo ni kweli? Kuna mtu kanidokeza kwamba ukifungua kurasa moja, waweza kwenda Kariakooo ukarudi kurasa bado haijafunguka, duh hiyo noma mtu wangu.. Naona we ndiyo upo hapo hapo katika uozo huo, pole we!--Mwanaharakati (majadiliano) 09:30, 26 Machi 2008 (UTC)Reply

Ronaldinho‎

hariri

We babu we, ndiyo umeandika nini katika kurasa hii ya Ronaldinho‎? Naomba uweke sawa kabla jembe halijapita...--Mwanaharakati (majadiliano) 09:34, 26 Machi 2008 (UTC)Reply

Haya nishamaliza kuiweka sawa ile makala uliotia ujuzi wako wa puli kama Ustadh Mikkidadi wa usiogope. Ila haitakiwi uandike vile ikiwa unauzoefu na uundaji wa makala katika Wikipedia. Siku nyingine ukijiona unataka kufanya majaribio tafadhali unaombwa utumie Sanduku la Mchanga kwa majaribio yako! Karibu sana..--Mwanaharakati (majadiliano) 10:29, 26 Machi 2008 (UTC)Reply

Re:Template:Mchezaji

hariri

Sikia we babu, template hiyo ipo sema bado haijamaliziwa. Endapo utaona una muda wa kuindeleza, basi fungua hapa ili uweze kuitazama na kuifanyia marekebisho kadhaa! Hapa kazi ipo...--Mwanaharakati (majadiliano) 09:45, 26 Machi 2008 (UTC)Reply

We master wa vijibwa, vipi umeiona hiyo template?--Mwanaharakati (majadiliano) 10:03, 26 Machi 2008 (UTC)Reply

Jamii ya wanasoka

hariri

Salam nyingi zikufikie Nd. Said wa Abdallah huko uliko Kiwalani kwa Gude! Unazungumzia jamii?? Jamii zikonyingi sana zenye kuhusu mpira!! Unaweza kuumba jamii kwa mujibu wa taratibu za Wachezaji kwa nchi. Kwa mfano unataka kuumba jamii ya Wanasoka wa Uingereza au Wanasoka wa Tanzania!! Kuhusu jamii ni mwenendo wa mwanamakala wa Wikipedia vile anavyoona kuumba jamii kwa mtililiko wa pamoja. Yaani kama unaandika kuhusu mambo ya soka, basi uandike jamii yenye kutaja maelezo sawa na soka! Angalia mifano:

  • Category:Wanasoka wa Tanzania
  • Category:Wanasoka wa Ujerumani
  • Category:Wanasoka wa Hispania

Na wengine wengi tu. Natumai utakuwa umenipata! Basi karibu sana..--Mwanaharakati (majadiliano) 13:25, 28 Julai 2008 (UTC)Reply

Global Akaunti

hariri

Saed, salam! Samahani kwa kukuchelewa kukujibu  Hebe jaribu hii:

Lakini baadaye itakupa hiari ya kuweka nywila na jina kamili la akaunti yako ili uweze kuingia katika miradi yoote! Jaribu, ukishindwa nijulishe!!--Mwanaharakati (Longa) 16:39, 24 Desemba 2008 (UTC)Reply

Mwanaharakati awe bureaucrat

hariri

Nimemteua Mwanaharakati achaguliwe kuwa msimamizi mkuu pamoja nasi (b'crat). Naomba upige kura kwenye ukurasa wa wakabidhi. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 08:11, 28 Mei 2009 (UTC)Reply


Kura ya kuamua juu ya wakabidhi waliopotea

hariri

Karibu kutembelea ukurasa wa wakabidhi na kuamua juu ya wenzetu waliopewa haki za wakabidhi lakini hawakuonekana tangu miezi mingi: Wikipedia:Wakabidhi#Kura_ya_kuondoa_wakabidhi_waliopotea. Tuliwahi kujadili swali hili mwaka uliopita (tazama kwenye ukurasa unaotajwa, juu ya pendekezo) ; sasa njia imeonekana. Kipala (majadiliano) 05:26, 1 Oktoba 2010 (UTC)Reply

Naomba ushirikiano wako!

hariri

Mpendwa, nakuomba uangalie baada ya siku 2,3 kurasa hizi mbili:

1. Wikipedia:Wakabidhi#Kusafisha_orodha_ya_Wakabidhi_mwaka_2014
2. Wikipedia:Ukurasa_wa_jumuia#Wiki_Indaba_2014

Kuhusu 1) napendekeza kuwachagua wakabidhi wapya na kuondoa wale waliomo katika orodha ya wakabidhi lakini hawakuwepo tangu miaka 2.

Kuhusu 2): nahitaji msaada na mawazo yenu. Nitashiriki kwenye mkutano wa Wikimedia mwezi wa Juni. Inaonekana mimi ndipo mchnagiaji wa pekee kutoka Wikipedia yetu. Ninajitahidi kupeleka mawazo ya jumuiya yetu. Naomba michango!

Nitaongeza karibuni mawazo yangu kuhusu mambo ninayoona kuwa na maana kwa mtazamo wangu. Ujumb huu natuma kwa wachangiaji wanaoonekana katika orodha ya wachangiaji hai waliochangia zaidi ya mara 3 katika siku 30 zilizopita!

Ndimi wako Kipala (majadiliano) 20:18, 13 Mei 2014 (UTC)Reply