Kiwalani ni mojawapo kati ya kata zilizopo katika wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam, nchini Tanzania, yenye postikodi namba 12108. Iko ndani ya jiji la Dar es Salaam na kupakana na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Kwa upande wa mashariki imepakana na barabara ya Nyerere, upande wa kusini imepakana na kituo cha reli ya TAZARA.

Kata ya Kiwalani
Kata ya Kiwalani is located in Tanzania
Kata ya Kiwalani
Kata ya Kiwalani

Mahali pa Kiwalani katika Tanzania

Majiranukta: 6°49′26″S 39°14′56″E / 6.82389°S 39.24889°E / -6.82389; 39.24889
Nchi Tanzania
Mkoa Dar es Salaam
Wilaya Ilala
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 40,049
Eneo la Kijiwe Samli transfoma au maarufu kwa Mzee Dieni.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 40,049 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2012, kitongoji kilikuwa na idadi ya wakazi wapatao 82,292.[2]

Kitongoji hiki kilianzishwa miaka ya 1970 baada ya watu kuhamishwa na serikali kutoka katika viwanja vyao sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam.

Mgawanyiko wa Kiwalani

hariri

Kiwalani ina mgawanyiko mkubwa sana, pia ina majina tofauti mengi tu, kama:

  1. Kiwalani Kariagogo
  2. Kiwalani Minazi Mirefu
  3. Kiwalani Bombom
  4. Kiwalani Kigilagila
  5. Kiwalani Yombo
  6. Kiwalani Deimasoko

Kwa upande wa Bombom, kidogo eneo lake limekaa vyema kwa kutokuwa na madimbwi mengi ya maji jinsi ilivyo upande wa Kiwalani Kigilagila. Kigilagila kuna maji mengi mno - hasa kipindi cha masika kuna hali mbaya kupita kiasi. Wakazi wengi wanaokalia maeneo ya shule ya msingi ya Kiwalani huwa tabuni kwa kipindi hicho: madimbwi, mitaro mibovu, mashimo yasiyo na mpangilio na upangiliaji usiofaa wa makazi ya watu. Kiwalani Minazi Mirefu kupo sawa na na Kijiwe Samli kwa sababu kumeinuka hivyo maji hayakai sana kama jinsi ilivyo kwa upande wa Kigilagila.

Deimasoko napo kunafanana kabisa na mfumo mpangilio mbovu wa makazi. Yaani, kupo hovyohovyo - kiasi kwamba nyumba zimebanana hadi kero. Madimbwi ya maji ni mengi mno kupita kiasi. Eneo hili malaria huwa juu sana kutokana na madimbwi yaliyopo huko. Kinachosabisha eneo la Kigiglagila kuwe na maji mengi, ni kwa sababu eneo la kule lilikuwa eneo la mashamba ya mpunga. Kwa namna moja au nyingine, Kiwalani yote lilikuwa eneo la mashamba ya mpunga. Ndiyo maana kila eneo lake limetapakaa majimaji.

Marejeo

hariri
  1. https://www.nbs.go.tz/
  2. "Sensa ya 2012, Kiwalani" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-08-18.
  Kata za Wilaya ya Ilala - Tanzania  

Bonyokwa | Buguruni | Buyuni | Chanika | Gerezani | Gongolamboto | Ilala | Jangwani | Kariakoo | Kimanga | Kinyerezi | Kipawa | Kipunguni | Kisukuru | Kisutu | Kitunda | Kivukoni | Kivule | Kiwalani | Liwiti | Majohe | Mchafukoge | Mchikichini | Minazi Mirefu | Mnyamani | Msongola | Mzinga | Pugu | Pugu Station | Segerea | Tabata | Ukonga | Upanga Magharibi | Upanga Mashariki | Vingunguti | Zingiziwa