Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:59, 18 Agosti 2021 (UTC)Reply

Tafsiri hariri

Salamu, tazama katika makala ilokuwa ikimuhusu Alan Edgar Stratford Johns , kwa wakati mwingine hakikisha katika makala yako hakuna tafsiri ya Kompyuta ama Kiswahili kisichokuwa kikieleweka,Amani Sana Idd ninga (majadiliano) 16:04, 1 Novemba 2021 (UTC)Reply


Jamii hariri

Salamu Suzan, tazama katika jamii unazoweka, ni vyema kuangalia kama jamii unayotaka kutumia inaendana na makala husika, kuna jammii ya Wanawake umeweka katika makala ya John Burra, kitu ambachgo inaharibu maana ya jamii katika makala husika,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 10:18, 2 Machi 2022 (UTC)Reply

Naona bado unaendelea kuchanganya jamii: riadha na badminton si mpira wa miguu. Pia miaka inayotajwa juu pengine ni tofauti na ile ya jamii. Hata kundi lenu ukiandika [[jamii:Arusha women in wiki]] ni tofauti na [[jamii:Arusha Women in Wiki]], hivyo haiingii. Uwe makini zaidi, hata kama ni kupunguza idadi ya kurasa. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:44, 8 Machi 2022 (UTC)Reply
Simama kwanza! Unaendelea kufanya makosa yaleyale. Napoteza muda mwingi kuyasahihisha!!! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:40, 8 Machi 2022 (UTC)Reply

Tafsiri hariri

Tazama katika makala hii https://sw.wikipedia.org/wiki/Deborah_Acquah , makala imekuwa na lugha ya Kiswahili ambayo ni ngumu kueleweka na kuna dalili ya makala yako kutumia mashine ya kutafisiri, heri kuirekebisha kwanza kabla ya kuendelea na uandishi wa makala nyingine, pia tazama Jamii unazoweka kama zipo sahihi,, na kabla ya kuchapisha makala yako ni bora uwe unaihakiki kwanza, Amani Sana Idd ninga (majadiliano) 10:28, 11 Machi 2022 (UTC)Reply

Taarifa ya kukuzuia!

Ndugu, imenibidi kukuzuia kwa sababu zinazotajwa chini. Wakati unapokuwa umezuiwa huwezi kuhariri isipokuwa penye huu ukurasa wako wa majadiliano. Unaweza kunijibu kwa kutumia “Email this user”.

Sababu ni kuwa umeingiza matini iliyopatikana kwa njia ya tafsiri ya kompyuta ikiwa na kasoro nzito ya lugha. Umearifiwa kwamba ni marufuku kumwaga matokeo ya google translate katika makala zetu. Wachangiaji wanaopuuza utaratibu huu wanasababisha hasara kubwa kwa Wikipedia yetu na kuwapa wengine kazi kubwa mno ya kusafisha makosa yao.

Bila shaka una nia nzuri kuchangia katika Wikipedia. Tutafurahi kushirikiana nawe lakini ni lazima ufuate utaratibu. Kazi yetu kama wakabidhi ni kulinda mradi huu.

Ukiwa tayari kufuata utaratibu pamoja na kupitia upya matini ulizozileta tayari, naomba uwasiliane nami kwa kufungua ukurasa wangu (bofya jina langu chini) na kuniandikia baruapepe kwa kubofya “Email this user” upande wa kushoto. Hapo nitaweza kukuruhusu tena. Hapo lazima uwezeshe njia kwa kufuata maelezo katika Wikipedia:Email.

Idd ninga (majadiliano) 10:34, 11 Machi 2022 (UTC)Reply

Tazama pia katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Dorra_Mahfoudhi kuna dalili nyingine kuwa umetumia tafsiri ya kompyuta, pitia tena na makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Grace_Anigbata, Amani Sana Idd ninga (majadiliano) 10:34, 11 Machi 2022 (UTC)Reply