Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Vyanzo!! hariri

Hu uni ujumbe kwa watumiaji wetu TORY66, Elisha the great, Simon waziri msika na ALLY ROCKSTAR 4000. Naona ya kwamba mnaleta makala kuhusu wachezaji wa mpira. Napenda kuwapongeza kwa kazi hii! Ni muhimu pia nina uhakika ya kwamba wasomaji wengi watafurahi kupata habari zao kwa lugha yetu ya Kiswahili. Lakini kuna kasoro 3 katika makala zenu:

1. Wakati mwingine mnasahau Jamii au hamweki jamii zote. Hasa mnasahau kutaja jamii ya nchi. Chini ya kila makala ziwepo jamii. Mfano: [[Jamii: Mbegu za wachezaji mpira]] na [[Jamii:Wachezaji wa mpira wa (NCHI)]]

2. hakuna interwiki (yaani kiungo kwa makala juu ya mtu yeye yule katika lugha nyingine). Fanya hivi: baada ya kumaliza makala na kuipakua utaona chini upane wa kushoto maneno Add links. Bofya hapo utaona madirisha 2; juu andika en na kuthebitisha English (enwiki). Dirisha la chini andika lemma (yaani jina la makala), thibitisha, tayari. Kuanzia sasa makala yako itaonekana kwa kila wikipedia kwa lugha yoyote.

3. hakuna vyanzo. Maana yake hakuna uthebitisho kama huyu mtu yuko kweli au kama habari mnazoleta zina uthebitisho wowote. Zamani hatujajali sana lakini sasa imekuwa muhimu zaidi maana Wikipedia yetu ya Kiswahili imepata wasomaji wengi kiasi. Una njia mbili Kwanza tunga kila makala pamoja na vichwa vya

==Tanbihi==
<references/>
na
==Marejeo ya Nje==

„Tanbihi“ ni nafasi ya tanbihi (footnotes) na alama ya <references/> itaonyesha hapahapa footnotes ulizoweka katika matini.
Marejeo ya Nje ni nafasi kutaja tovuti, kitabu na kadhalika.
Kama makala ya Kiingereza ina sehemu ya "External links" basi bofya edit source, nakili yote na uiweke chini ya makala ya Kiswahili, chini ya kichwa "Marejeo ya Nje" .
Angalia habari juu ya mhusika ndani ya makala ya Kiingereza. Je kuna tanbihi? Kama ziko, bofya edit source (kuna fomati nyingine ambazo hatuwezi kuhamisha kwetu). Angalia kama reference inaanza na alama <ref>. Kama ni hivyo nakili reference yote kuanzia <ref> hadi alama ya <ref/> na ingiza mahali pake kwenye matini baada ya habari inayothibitishwa kwa chanzo hiki.

Angalia mfano wa makala Phil Jagielka nilipoongeza tanbihi na viungo vya nje. Naomba A) msisahau kuanzia sasa kuongeza sehemu hizi! na B) pia naomba mrudie makala mlizoweka tayari na kuboresha makala.

Mkiwa na swali mwulize Riccardo au mimi. Kipala (majadiliano) 19:04, 27 Agosti 2018 (UTC)Reply