Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Twamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo - hata kuitafsiri kutoka katika Wikipedia kwa lugha nyingine. Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wa sanduku la mchanga. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike pekee kwenye ukurasa wako wa mtumiaji baada ya kufungua akaunti. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho. Ujue miiko: usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje wala matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo). Karibu sana!

Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non speaker better first communicate with one of our admins who will advise you. You find them at Wikipedia:Wakabidhi. And btw: NEVER post computer translated texts (like google-translate, mediawiki Content Translation etc.) nor copied texts/images from other webs to this site! And do not use links to commercial pages.

Kipala (majadiliano) 10:55, 2 Mei 2016 (UTC)

AsanteEdit

Asante Bwana Kipala. Mimi ni mwanagenzi hapa Kenya katika shule ya msingi na ninarudi skulini mtondo.Trunzep (majadiliano) 17:49, 2 Mei 2016 (UTC)

Haki za usimamizi WiktionaryEdit

Salaam Ndugu RazorTheDJ! Ndugu, ili uweze kuwa msimamizi kule Wikamusi inabidi uende hapa watakupa usimamizi wa muda tu. Ukifanya vizuri, wanaweza kukupa urasimu au usimamizi wa kudumu! Karibu sana.--MwanaharakatiLonga 07:00, 12 Novemba 2016 (UTC)

Done! Now let's wait for their replies.. I have played my part.--MwanaharakatiLonga 09:35, 12 Novemba 2016 (UTC)


Michango na ukabidhiEdit

Ndugu Trunzep, uliuliza hapo na pale na kusema unapenda kuwa mkabidhi wa sw-wkipedia au wikikamusi. Kwa sasa naona uonyeshe uwezo wako kuchangia katika kuhariri na kutunga makala. Kwa kawaida tumepokea wahariri waliochangia vema na kwa muda na hivyo walionekana wameelewa kazi. Naona wewe ni Mkenya na kwa kweli tunakosa makala nyingi sana kuhusu mambo ya Kenya. Nitafurahia kuona michango yako. Naona hadi sasa umechangia 3,4 katika wikikamusi na pia kidogo katika wikipedia. Nitafurahi sana kuona jinsi unavyoendelea. Fanya tu, baadaye tuongee kuhusu mengine. Kipala (majadiliano) 12:14, 12 Novemba 2016 (UTC)

TafsiriEdit

Tafadhali, ndugu, ukitaka kuchangia Wikipedia ya Kiswahili usitegemee kifaa cha kutafsiria. Afadhali maneno 10 yanayoeleweka kuliko kurasa nyingi za Kiswenglish kama huu juu ya Vera. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:57, 17 Novemba 2016 (UTC)

Kuhusu hayo Riccardo, nafanya marekebisho makubwa mathalan nimeona mashine hiyo si 'accurate'. Asante kwa kuniarifu.-- Trunzep (majadiliano) 08:18, 17 Novemba 2016 (UTC)

Majimbo ya Uchaguzi / Maeneo bungeEdit

Asante kwa kuingiza data mpya kuhusu jimbo la Limuru. Je, unaweza kufanya vilevile kwa majimbo mengine? Pia nina swali: huko Kenya mnasemaje zaidi: jimbo la uchaguzi au eneo bunge? Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:38, 4 Machi 2019 (UTC)

Asante tena kwa jibu lako. Nafurahi kusikia wewe ni mwanafunzi wa kidato cha 3 kama wachangiaji wengi wa Wikipedia kutoka sekondari ninayoiangoza huku Morogoro. Msonge mbele, mtupokee sisi wazee katika kuendeleza elimu kwa Kiswahili! Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:04, 7 Aprili 2019 (UTC)