"Make Me Better" ni single ya tatu ya msanii Fabolous' kutoka katika albamu yake ya From Nothin' to Somethin'. Wimbo umemshirikisha mwimbaji machachari wa R&B Ne-Yo, lakini alikuwa akipiga sehemu za vibwagizo tu. Wimbo umetayarishwa na Timbaland.

“Make Me Better”
“Make Me Better” cover
Single ya Fabolous na Ne-Yo
kutoka katika albamu ya From Nothin' to Somethin'
Imetolewa 9 Juni 2007 (ulimwenguni)
Muundo CD single (ulimwenguni)
Digital download (global)
Vinyl single (North America)
Imerekodiwa Brooklyn, New York, Marekani na Hollywood, Los Angeles, California, Marekani
Aina Hip hop
Urefu 4:13
Studio Def Jam Records
Mtunzi John Jackson
Shaffer Smith
Mtayarishaji Timbaland
Certification Platinum (RIAA)
Mwenendo wa single za Fabolous
"Return of the Hustle"
(2007)
"Make Me Better"
(2007)
"Baby Don't Go"
(2007)
Mwenendo wa single za Ne-Yo
"Sexual Healing" "Make Me Better"
(2007)
"Hate That I Love You"
(2007)

Yaliyomo Wimboni

hariri

Timbaland alidokezea kidogo kuhusu wimbo na alisema kwamba:

"biti linasauti ya kipekee na nyuzi zake ni nzuri sana ambazo zitakuja kutumika katika nyimbo zingine hapo baadaye".

Nyuzi za wimbo huu ni sampuli kutoka kwa Sherine "Al Sa'ban Aleh". Sampuli kama hii ilishawahi kutumiwa na RZA katika wimbo wa Raekwon wa mwaka 1995 ("Rainy Dayz"). Funkmaster Flex naye alishawahi kuitumia kwa ajili ya michano huru ya Busta Rhymes ya The Mix Tape Volume 1: 60 Minutes of Funk.

Wimbo huu umemfanya Fab ajikute katika hali ya kawaida, kwa kuongea na mademu. Kwa mujibu wa mashairi, Fab na Ne-Yo wanawaambia mademu zao kwamba wanalazimika kuhesabiwa kivyao — lakini wawe na mademu zao, yaani wao ni wabora zaidi.

"Unamtaka demu ambaye aliyetimia na anayekufanya ujisikie vyema," alielezea. "Humtaki demu anayekuletea malumbano na hasara zaidi, siyo. ... Unamtaka demu gani, pale unapotembea mtaani na tai yako imefyatuka, yeye awe anairejesha. .... Huyo ndiye [demu] ninayemtafuta. Awe maarufu au asiwe-maarufu wala haijalishi. Unamhitaji mtu ambaye utaweza kuungana naye. "Inanigusa kila mahali," Fab akaongezea kibwaizo wimboni. "Hii ni rekodi poa, jumlisha rekodi iliyotimia, rekodi ya taifa yote kwa moja. ... Nimechezea wachuchu kwa wiki mbili zilizopita, na walikuwa kama, 'Mi' ninaelezea kwa ufupi tu kwamba: "Yo, gashi, unanifurahisha. Nipo poa, Nina paa na ye--, lakini sisi sote, tunapendeza kishenzi yaani." "Mabishoo wanaweza wakaitaka hii — inawapatia mtawasha. Ninatumai ya kwamba itafanya kazi katika hali zote."

Kwa bahati mbaya wimbo mzima ulivuja katika mtandao mnamo tar. 9 Aprili 2007.

Muziki wa Video

hariri

Video yake ilitolewa mnamo tar. 23 Mei 2007. Unaweza kuitazama kwa kupitia anwani hii hapa. Roselyn Sánchez ameonekana katika video akiwa kama kipenzi cha Fabolous. Video ilianza kurushwa hewani na BET mnamo tar. 25 Mei 2007. Video hii imeuzishwa sura rapa kama Red Cafe na Dwight Freeney kama mtu aliyezinguliwa na mlevi.

Mafanikio katika Chati

hariri

Kwa kufuatana na tarehe ya kutolewa 9 Juni 2007, single ilipata kuingia katika chati za Billboard Hot 100 na kushika nafasi ya 96 na kisha baadaye 8 [1]. Single ilitumia wiki 14 kwa kushika nafasi ya kwanza katika Billboard Hot 100 Rap Tracks. Hii ni rekodi ya chati za 2006 na 2007.

Mnamo mwezi wa Januari 2008 toleo la la Gazeti la VIBE, limeipa jina kibao cha "Make Me Better" katika orodha ya nyimbo 44 bora za mwaka wa 2007[2].

Muundo

hariri
Albamu
  1. "Make Me Better" (toleo la albamu) akimshirikisha Ne-Yo
Promo
  1. "Make Me Better" (haririo la redio) akimshirikisha Ne-Yo
  2. "Make Me Better" (vyombo vitupu)
Remix zake
  1. "Make Me Better" (Greg Street Remix #1) akimshirikisha Jagged Edge (Remix Rasmi)
  2. "Make Me Better" (Greg Street Remix #2) akimshirikisha Lil' Mo [3]
  3. "Make Me Better" akimshirikisha Angela Via[4]

Chati zake

hariri
Chati (2007) Nafasi
iliyoshika
U.S. Billboard Hot 100[1] 8
U.S. Billboard Hot R&B/Hip-Hop Songs 2
U.S. Billboard Hot Rap Tracks 1
U.S. Billboard Pop 100 14
Canadian Hot 100 79

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 "Fabolous f Ne-Yo Make Me Better global chart positions and trajectories". aCharts.us. Retrieved 30 Juni 2007.
  2. "The 44 Best Songs of 2007". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-04-14. Iliwekwa mnamo 2009-04-28.
  3. http://www.youtube.com/watch?v=nMUhmEJdAB4 Make Me Better Remix f Lil Mo
  4. http://www.youtube.com/watch?v=MQ0qyzbiimg Agela Via on Fabolous remix

Viungo vya Nje

hariri