John David Jackson (amezaliwa tar. 18 Novemba 1977) ni msanii wa rekodi za hip hop kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama Fabolous. Alikulia mjini Brooklyn huko New York City, alikuwa mmoja kati marapa wa East Coast ambao waliathiriwa na muziki wa Southern hip hop. Moja kati ya kazi zake za awali ambayo ilimletea umaarufu ni pamoja na "Can't Deny It" mnamo 2001, kutoka katika albamu yake ya kwanza ya Ghetto Fabolous. Fabolous ametoa albamu tano, ambazo zote kwa ujumla zimeuza nakala zaidi ya milioni tatu huko nchini Marekani.[1]

Fabolous
Fabolous at Sirius Satellite Radio in 2007
Fabolous at Sirius Satellite Radio in 2007
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa John David Jackson
Aina ya muziki Hip hop
Kazi yake Rapa, mtunzi wa nyimbo
Miaka ya kazi 1998–mpaka sasa
Studio Desert Storm, Def Jam
Ame/Wameshirikiana na Jagged Edge, Lil Mo, Nate Dogg, Mike Shorey, Ne-Yo, Pharrell Williams, Red Cafe, The-Dream, Young Jeezy

Maisha na kazi hariri

Maisha ya awali na mwanzo wa kazi hariri

Fabolous alizaliwa John David Jackson mnamo tar. 18 Novemba 1977, na wazazi wenye asili ya Kiafrika-Kiamerika na Kidominika.[2][3] Alikulia huko Bedford-Stuyvesant jirani kidogo na Brooklyn, New York.[4][5] Wakati anasoma elimu ya juu, Fabolous akaanza kujifua katika masuala ya muziki wa rap. Alialikwa kurap moja kwa moja kipindi cha redio cha DJ Clue na kwenye WQHT Hot 97, ambapo kulimpatia uwezo wa kuweza kuingia mkataba na studio ya Desert Storm Records.[6] Alipata kushirikishwa kwenye mamixi tepu kibao ya DJ Clue na mamixi tepu mengine mingi tu ya wasaniii wa Roc-A-Fella.

Diskografia hariri

Marejeo hariri

  1. Hilliard, Chloe A. (2008-02-05). The Fabolous Life. The Village Voice 1–4. New Times Media. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-01-01. Iliwekwa mnamo 2009-03-01.
  2. Birchmeier, Jason. Fabolous - Biography. Allmusic. Iliwekwa mnamo 2008-10-18.
  3. Fabolous. Hip Hop Galaxy. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-12-08. Iliwekwa mnamo 2008-02-28.
  4. Mfuni, Tanangachi; Gould, Joe; Lemire, Jonathan. "Rapper Fabolous' friend is fatally stabbed, according to club area toll", New York Daily News, 2007-11-24. Retrieved on 2008-02-28. Archived from the original on 2009-02-08. 
  5. Vasquez, Emily. "Brooklyn-Born Rapper Is Arrested After Being Shot", The New York Times, 2005-10-18. Retrieved on 2007-10-07. 
  6. Reid, Shaheem (2001-05-17). Fabolous Gets A Clue, Records Debut Album For Mixtape King. MTV News. Iliwekwa mnamo 2009-07-31.
  7. http://www.mtv.com/news/articles/1627964/20091209/fabolous.jhtml

Viungo vya Nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fabolous kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.