Malika Domrane

Malika Domrane (alizaliwa 12 Machi, 1956 huko Tizi Hibel) ni mwimbaji nchini Algeria, mwenye asili ya Kabylie . [1]

Malika Domrane

MaishaEdit

Domrane alianza kuimba katika kwaya yake ya shule ya upili huko Tizi Ouzou . Mnamo 1969 alishinda medali ya dhahabu kwenye tamasha huko Algeria. Baada ya kuhitimu uuguzi, alianza kazi hospitalini lakini baada ya muda mfupi aliamua kujitosa katika kuimba, ambapo ni kinyume na desturi za familia na kijiji chake.

Mnamo mwaka 1979, alienda Ufaransa kutoa albamu yake ya kwanza, Tsuha. Baadae alichapisha albamu kadhaa, na nyimbo zilizofananishwa na tamaduni za kifeministi na lugha ya Waberber . Kuanzia 1994, aliamua kuishi Ufaransa na familia yake.

AlbamuEdit

MarejeoEdit

  1. Naylor, Phillip Chiviges (2006). Historical dictionary of Algeria. Scarecrow Press, 458. ISBN 978-0-8108-5340-9.