Kuzi (samaki)

(Elekezwa kutoka Mambanguma)
Kuzi
Kuzi milia-mipana (Atherinomorus lacunosus)
Kuzi milia-mipana (Atherinomorus lacunosus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Atheriniformes (Samaki kama kuzi)
Familia: Atherinidae (Samaki walio na mnasaba na kuzi)
Risso, 1827
Ngazi za chini

Jenasi 13 na spishi 74, 9 katika Afrika:

Kuzi, dagaa, makame kuoza au mambanguma ni samaki za baharini na maji baridi za familia Atherinidae katika oda Atheriniformes. Wanatokea katika kanda za wastani mpaka tropiki.

Kuzi ni wadogo, spishi kubwa kabisa, kuzi wa Kalifornia (Atherinopsis californiensis), anafikia urefu wa sm 44 lakini wengi zaidi ni chini ya sm 20 na kadhaa hazikuandikwa kwa zaidi ya sm 5. Kwa kawaida mwili umerefuka. Hulka bainifu zinajumuiya mapezimgongo mawili yaliyojitokeza sana, lile la kwanza likiwa limeundwa kwa miiba kinamo na lile la pili likiwa na mwiba mmoja unaofuatiwa na tindi laini. Pezimkungu pia lina mwiba mmoja unaofuatiwa na tindi laini. Mapeziubavu huwa juu na hakuna mrabafahamu. Kuna mlia mpana wa rangi ya fedha mbavuni. Magamba ni makubwa kiasi.

Hula planktoni-wanyama. Spishi kadhaa, k.m. kuzi milia-mipana (Atherinomorus lacunosus), huvuliwa kibiashara.

Spishi za Afrika

hariri

Marejeo

hariri
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kuzi (samaki) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.