Mana (kwa Kiebrania מָ‏ן) ni chakula kilichotumiwa na Waisraeli walipotangatanga katika jangwa la Sinai miaka 40 mfululizo baada ya kutolewa na Musa nchini Misri walipokuwa wananyanyaswa.

Mana ikikusanywa kadiri ya mchoraji James Tissot.

Habari hizo zinapatikana katika vitabu vingi vya Biblia (hasa Kutoka 16:1-36 na Hesabu 11:1-9) na vilevile katika Kurani 5:27.

Pamoja na maelezo mbalimbali yaliyotolewa na wataalamu kuhusu asili ya chakula hicho, kwa imani kilitazamwa kama ishara ya pekee ya Mungu kuwashughulikia watu wake.

Yesu alikitumia hicho pia kujitambulisha ni nani kwa binadamu wote: "Mimi ndimi chakula cha kweli kilichoshuka kutoka mbinguni" (Yoh 6).

Fumbuzi za kisayansi hariri

Wanasayansi wamejaribu kufumbua kitu hicho cha mana. Ufumbuzi mmoja ni kwamba mana ni sandarusi ya mchamwino, mti unaomea sana katika Rasi ya Sinai. Sandarusi hii ni tamu na ikiwa imekauka ina rangi ya hudhurungi.

Ufumbuzi mwingine ni kwamba mana ni mchozo wa wadudu kama vidukari na wadudu-gamba, k.m. mdudu-gamba wa mchamwino (Trabutina mannipara). Katika hali ya hewa moto na kavu ya Rasi ya Sinai mchozo huo hukauka haraka. Fuwele za mchozo huo ni tamu na zina rangi ya manjano au hudhurungi. Mara nyingi michozo kama huo huitwa mana pia.

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mana kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.