Mateus Alberto Contreiras Gonçalves (alizaliwa 7 Machi 1983 Jijini Luanda), ambaye anajulikana kwa jina maarufu kama ‘’’Manucho.’’’ ni mchezaji wa Soka wa FA kutoka Angola ambaye sasa hivi anaichezea timu ya Real Valladolid katika La Liga.[1]. Alitoka Petro Atletico, kuhamia Manchester United mnamo Januari 2008.[2][3][4]. Hata hivyo kabla ya kuichezea Manchester United] alinunuliwa kwenda kuichezea klabu ya Ugiriki ya Panathinaikos kwa msimu uliosalia wa 2007-08 kufuatia mizozo kuhusu kupata kibali cha kazi cha Ufalme wa Muungano. .[5]. Manucho alipata kibali hicho punde na akarejea Manchester United kwa mazoezi kabla ya kuanza msimu mnamo Julai 2008,[6] na akaanza kuichezea klabu hiyo kwa mara ya kwanza wakati wa mechi yake dhidi ya Middlesbrough mnamo 23 Septemba 2008 katika kombe la Ligi ya Ubingwa. Kwa kukosa nafasi katika timu ya kwanza jijini Old Trafford, alijiunga na klabu ya Hull City kama mkopo hadi mwisho wa msimu wa 2008–09.[7]. Aliposhindwa kujiunga na timu ya kwanza ya (Manchester United) aliamua kuihamia klabu ya Real Valladolid mnamo Julai 2009. Yeye pia ni mchezaji katika Timu ya Taifa ya Angola.

Manucho akicheza Mpira
This is a Portuguese name; the first family name is Contreiras and the second is Gonçalves.
Manucho
Youth career
1997–1999Flamenguinhos
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
1999–2002Benfica de Luanda12(5)
2002–2008Petro Atlético78(34)
2008–2009Manchester United1(0)
2008Panathinaikos (loan)7(4)
2009Hull City (loan)13(2)
2009–Real Valladolid13(2)
Timu ya Taifa ya Kandanda
2006–Timu ya Taifa ya Kandanda ya Angola30(15)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 18:54, 5 Januari 2010 (UTC).

† Appearances (Goals).

‡ National team caps and goals correct as of 18:54, 5 Januari 2010 (UTC)

Kazi hariri

Manucho alianza kucheza soka katika klabu ya vijana ya Flamenguinhos kutoka Terra Nove jijini Luanda ambapo alikuwa akiishi. Kupitia ukufunzi wa babake Alberto Gonçalves, ambaye alikuwa Kocha, Manucho alijiimarisha kama mchezaji wa wingi ya Kushoto, na akuwa mmoja wa nyota wa klabu hiyo.

Kazi ya Mwanzo hariri

Baada ya kuwa mchezaji wa kulipwa Manucho alitia kandarasi na klabu ya Benfica de Luanda, klabu ya kati ya Ligi ya Angola

Hatimaye alihamia klabu ya Petro Atlético jijini Luanda ambapo alikuwa na ugumu kuingia na kutambulika kutokana na kuwepo kwa mshambulizi Flávio Amado]]. Baada ya Flávio kujiunga na klabu ya Misri ya Al-Ahly, Manucho alianza kujikuza katika nafasi hiyo akifunga mabao 16 mnamo 2006 na 15 mnamo 2007.

Mnamo 21 Desemba 2007, ilitangazwa kuwa Manucho alikuwa amekubali kutia mkataba kandarasi na Mabimgwa wa Ligi ya Premier ya Uingereza Manchester United. Alijiunga na klabu hiyo mnamo Januari 2008 katika kandarasi ya miaka mitatu. Manucho alikuwa katika majaribio ya wiki tatu na klabu hiyo kabla ya tangazo hilo ambapo alifaulu kumvutia meneja wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson.[2][3][4]

Panathinaikos hariri

Mnamo 31 Januari 2008, Manujo alikodishwa kwa klabu ya Panathinaikos ya Ugiriki kwa msimu uliobakia kutokana na mizozo kuhusu upataji wa kibali cha kazi nchini Uingereza. Lengo lake lilikuwa kupata ujuzi wa Timu ya Kwanza. .[5][8][9]. Meneja wa Manchester United Alex Ferguson alizitangaza habari za kukodishwa kwake mnamo 1 Februari 2008. Kipindi cha kukodishwa kwake kilianza punde baada ya Kutimuliwa kwa Angola kutoka Kombe la Mataifa Bingwa Barani Afrika na Misri .[10].

Manucho alifunga katika mechi yake ya kwanza katika klabu hiyo wakati wa ushindi dhidi ya Larissa.[11].

Pia alifunga mabao matatu katika mashindano sita ambayo ayaliisaidia timu hiyo kufuzu kucheza katika nafasi zilizosalia barani Uropa.

Manchester United hariri

Mnamo mwisho wa msimu wa 2007-08, Manucho alirejea Manchester United kwa mazoezi kabla ya mwanzo wa msimu na wakati klabu hiyo ilipozuru Afrika Kusini. Hata hivyo alipata jeraha baya ambalo lilimzuia kucheza katika mechi hizo za mazoezi[12]. Mnamo Agosti 2008, klabu hiyo ilithibitisha kuwa wamemwandikishia Manucho kibali cha kazi upya ili aendelee kuwachezea.[13]. Alikipata kibali hiki mnamo 28 Agosti 2008. ,[14].[15]. Manucho alikabidhiwa shati ya nambari 26 kwa msimu wa 2008-09. ingawa ilisemekana alikuwa na jeraha na ahangeweza kucheza, aliingia katika timu ya kwanza kwa mara ya kwanza kama mchezaji wa kubadilishwa wakati ea mechi dhidi ya Middlesbrough.. Mechi hiyo iliisha huku Manchester ikishinda 3-1. Manucho alicheza katika Ligi ya Premier mara ya kwanza mnamo 15 Novemba 2008 kama mchezaji wa kubadilishwa mnamo dakika ya 74 katika mechi ya nyumbani dhidi ya Stoke City FCstoke City. Dakika 10 baada ya kuingia, Manucho alikuwa kati ya mashambulizi yaliyozaa bao ambalo lilifungwa na by Danny Welbeck.[16] .

Mnamo 18 Desemba 2008, Manucho aliifungia klabu hiyo bao lake la kwanza, baada ya kugeuza pasi ya Magnus Wolff Eikrem kimyani. Bao hilo liliipatia sare ya 1-1 katika mechi hiyo dhidi ya Everton.[17].

Hull City hariri

Kwa uhaba wa fursa aliokuwa nao katika timu ya kwanza ya Manchester United FC, Manucho aliamua kujiunga na klabu ya Hull City kwa kukodishwa.kwa msimu uliosalia wa 2008-09.[7]. Alipata kibali cha kazi siku hiyo na kucheza kama mchezaji wa benchi katika mechi iliyoshindwa na Arsenali 3-1 mnamo 17 Januari 2009. .[18]. Mnamo 4 Machi 2009, alifunga bao lake la kwanza kwa Ligi ya Premier kwa Hull City. Bao hili la dakika ya mwisho liliipa Hull City ushindi wa 1-0 ugenini Dhidi ya Fulham.[19]

Real Valladolid hariri

Baada ya msimu mrefu akiwa na Hull, Mnamo 17 Julai 2009, Manchester United ilikubali kumuuza mchezaji huyo kwa klabu ya Uhispania ya Real Valladolid. Alitia mkataba kandarasi ya miaka mitano na klabu hiyo na akathibitishwa kuwa mchezaji wa Real Valladolid mnamo 20 Julai 2009. 13 Septemba 2009, aliifungia timu hiyo bao lake la kwanza katika mechi ambao ilishindwa na Valencia 4-2. Hatimaye alingoja hadi Desemba tarehe 5 2009 kufunga bao jingine ambalo liliwapa alama moja ya muhimu wakicheza ugenini dhidi ya Sevilla CF.

Kazi ya Kimataifa hariri

Manucho huichezea Angola katika mechi za kimataifa. Alikuwa katika kikosi kilichofuzu kwa Mechi za Mataifa Bingwa Barani Afrika za 2008.

Mnamo Januari 2008 aliifungia Angola bao la kwanza katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Afrika Kusini, na pia kufunga mabao mawili dhidi ya Senegali ambayo iliishia ushindi wa mabao 3-1. Manucho pia alifunga bao la pekee katika ushinde wao wa 2-1 dhidi ya Misiri. Ingawa ushinde huo uliwatimua kutoka mashindanoni, bao la Manucho kutoka umbali wa yadi 25 lilisemwa kuwa bao la mechi hiyo".[20]. Mwishoni mwa mashindano hayo, Manucho aliorodheshwa miongoni mwa wachezaji 11 bora (Timu ya Wachezaji 11 bora zaidi katika kila nambari)[21].

Katika Mechi a Kombe la Mataifa Bingwa Barani Afrika za 2010 zinazoendelea, alifunga bao la penalti katikka mechi ya ufunguzi ya Angola dhidi ya Mali ambayo ilishia sare ya 4-4.

Virejeleo hariri

 1. "Striker Manucho to leave Man Utd", BBC Sport, British Broadcasting Corporation, 17 Julai 2009. Retrieved on 17 Julai 2009. 
 2. 2.0 2.1 "Man Utd to sign striker Manucho", BBC Sport, 21 Desemba 2007. Retrieved on 21 Desemba 2007. 
 3. 3.0 3.1 "Boss reveals new signing", ManUtd.com, Manchester United, 21 Desemba 2007. Retrieved on 21 Desemba 2007. 
 4. 4.0 4.1 "Fergie reveals surprise deal", skysports.com, British Sky Broadcasting, 21 Desemba 2007. Retrieved on 21 Desemba 2007. 
 5. 5.0 5.1 "Manucho set for Greek loan move", BBC Sport, 31 Januari 2008. Retrieved on 1 Februari 2008. 
 6. "Manucho given Man Utd go-ahead", BBC Sport, 3 Septemba 2008. Retrieved on 3 Septemba 2008. 
 7. 7.0 7.1 "Hull snap up Manucho from Man Utd", BBC Sport, 16 Januari 2009. Retrieved on 16 Januari 2009. 
 8. "United starlet heads for Greece", skysports.com, British Sky Broadcasting, 31 Januari 2008. Retrieved on 31 Januari 2008. 
 9. "Manucho close to loan deal", ManUtd.com, Manchester United, 1 Februari 2008. Retrieved on 1 Februari 2008. 
 10. Thompson, G; Bostock, A. "Boss explains Manucho loan deal", ManUtd.com, Manchester United, 1 Februari 2008. Retrieved on 1 Februari 2008. 
 11. Spender, Barney. "Soccer-Manucho off the mark as Panathinaikos stay clear", Reuters UK, Thomson Reuters, 9 Machi 2008. Retrieved on 17 Januari 2009. 
 12. "Manucho Injury To Force Fergie's Hand?", Goal.com, 6 Julai 2008. Retrieved on 16 Julai 2008. Archived from the original on 2008-07-16. 
 13. "Ferguson to give Campbell chance", BBC Sport, 3 Agosti 2008. Retrieved on 3 Agosti 2008. 
 14. "Manucho close to Reds break", Manchester Evening News, M.E.N. Media, 28 Agosti 2008. Retrieved on 28 Agosti 2008. 
 15. "Reds line up for team photo", ManUtd.com, Manchester United, 28 Agosti 2008. Retrieved on 28 Agosti 2008. 
 16. Barder, Russell. "Man Utd 5-0 Stoke", BBC Sport, 15 Novemba 2008. Retrieved on 15 Novemba 2008. 
 17. Bartram, Steve. "Reserves: Everton 1 United 1", ManUtd.com, Manchester United, 18 Desemba 2008. Retrieved on 15 Januari 2009. 
 18. Ashenden, Mark. "Hull 1-3 Arsenal", BBC Sport, 17 Januari 2009. Retrieved on 17 Januari 2009. 
 19. Sanghera, Mandeep. "Fulham 0-1 Hull City", BBC Sport, 4 Machi 2009. Retrieved on 4 Machi 2009. 
 20. Whyatt, Chris. "Live - Africa Cup of Nations", BBC Sport, 4 Februari 2008. Retrieved on 4 Februari 2008. 
 21. "CAF names Best XI for Ghana 2008 ACN", cafonline.com, Confederation of African Football, 10 Februari 2008. Retrieved on 11 Februari 2008. Archived from the original on 2008-02-13. 

Viungo vya Nje hariri