Kombe la Mataifa ya Afrika

Kombe la Mataifa ya Afrika ni shindano kuu la soka la kimataifa katika bara la Afrika. Shindano hilo husimamiwa na Confederation of African Football (CAF), na lilichezwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1957. Tangu mwaka wa 1968, shindano hilo hufanyika baada ya miaka miwili. Mabingwa wa FIFA Confederations Cup walifuzu katika shindano hilo.

Kombe la Mataifa ya Afrika
Founded1957
RegionAfrica (CAF)
Current championsKigezo:Senegal
Most successful team Misri (7 titles)

Mwaka wa 1957 kulikuwa na mataifa matatu yaliyoshiriki katika shindano hili ambayo ni: Misri, Sudan na Ethiopia. Afrika ya Kusini walikuwa washiriki katika shindano hili lakini walizuiwa kutokana na sera za ubaguzi nchini humo.[1] Tangu wakati huo, shindano hilo limeenea, na kusababisha michuano ya kufuzu. Idadi ya walioshiriki katika fainali ya shindano hili ilifika 16 katika mwaka 1998 (timu 16 zilikuwa zishiriki katika shinano hili mwaka wa 1996 lakini Nigeria walijitoa na kubakia timu 15), na tangu wakati huo, imebaki kuwa timu 61 ndizo zinashiriki katika shindano hili. Timu hizi hugawanywa katika vikundi ambavyo kila kundi kina timu nne ambapo timu mbili bora katika kila kundi ndizo zinafaulu katika hatua ya ya pili.

Misri ndiyo taifa lililofanikiwa zaidi katika historia kombe hili kwa kuwa na rekodi ya kushinda kombe hili mara sita. Ghana na Kamerun wameweza kunyakuwa ubingwa mara nne. Nyara tatu tofauti zimetunzwa katika historia ya shindano hili. Ghana na Kamerunwameshinda matoleo mawili ya kwanza baada ya kila timu kushinda shindano hili mara tatu mfululizo. Nyara iliyo sasa ilitunzwa mara ya kwanza mwaka wa 2002.

Historia

hariri

1950-60: uenezaji wa shindano la ANC

hariri

Chimbuko la Kombe la Mataifa ya Afrika lilikuwa mnamo tarehe Juni 1956, wakati uundaji wa Confederation of African Football ulipendekezwa katika mkutano wa tatu wa bunge la FIFA mjini Lisbon. Kulikuwa na mipango ya haraka kwa mashindano ya mataifa ya bara kufanyika, na mwaka wa 1957 mwezi wa Februari shindano la kwanza la Kombe la Mataifa ya Afrika lilifanyika mjini Khartoum, Sudan. Hakukuwa na mechi za kufuzu katika shindano hili , kwani uwanja ulikuwa na mataifa manne ambao ndio wanzilishi wa CAF (Sudan, Misri, Ethiopia, na Afrika ya Kusini). Kukataa kwa Afrika ya Kusini kupeleka kikosi chenye wachezaji wa rangi tofauti katika ushindani kulisababisha wao kuadhibiwa na Ethiopia iliweza kufuzu katika fainali .[2] Kutokana na tukio hilo mechi mbili ndizo zilizochezwa na Misri kuwa bingwa wa kwanza katika bara baada ya kushinda Sudan katika nusu fainali na Ethiopia katika fainali. Miaka miwili baadaye, Misri ndiyo ilikuwa mwenyeji wa pili wa ANC mjini Cairo ambapo timu zile tatu ndizo zilishiriki .Kama mwenyeji na bingwa tetezi Misri iliweza kushinda baada ya kuwalaza sudan katika fainali.

Shindano hili lilienea na kuwa na timu tisa ambazo zilishiriki. Shindano hili la tatu la ANC mwaka 1962lilikuwa mjini Addis Ababa, na kwa mara ya kwanza kulikuwa na mechi za kufuzu ambapo timu nne zilifuzu kupigania ubingwa. Ethiopia kama mwenyeji Misri kama bingwa tetezi zilipata fursa ya kufaulu mara moja, na kuungwa na Nigeria na Tunisia katika timu nne za mwisho zilizo waania ubingwa. Misri iliweza kucheza fainali kwa mara ya tatu lakini Ethiopia waliwezakushinda, baada ya kupiga Tunisia katika semifinali nakulaza Misri katika muda wa ziada.

1960: Utawala wa Ghana

hariri

Katika mwaka 1963, Ghana ilishiriki kwa mara ya kwanza katika shindano hili , na iliweza kunyakua ushindi baada ya kuilaza Sudan katika fainali. iliweza kunyakuwa ubingwa miaka miwili baadaye nchini Tunisia -ikifikia mafanikio ya Misri kama bingwa wa misimu miwili - na kikosi ambacho kilikuwa na wachezaji wawili tu kutoka timu ya 1963.[3]

atika shindano la 1968 ilibidi mpango wa mchuano huo ubadilike na kuongeza hadi timu 8 zitakazo faulu kati ya timu 22 zilizofaulu katika raundi ya hapo awali. Timu zilizofaulu ziligawanyishwa katika makundi mawili kila kundi likiwa na timu nne ambazo zilicheza michezo ya mizunguko ambapo timu mbili bora zaidi katika kila kundi zilifaulu katika nusu fainali. Mfumo huu uliendelea kutumika katika fainali hadi mwaka wa 1992. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliweza kushinda baada ya kuwachapa Ghana. Kuanzia mwaka wa 1968 shindano hili limekuwa likitendeka baada ya miaka miwili katika miaka iliyo sawa. Mchezaji wa mbele wa Ivory Coast, Laurent Pokou aliongoza kwa mabao katika michuano ya 1968 na 1970 kwa mabao sita mwaka wa 1968 na mabao nane katika mwaka wa 1970 na kuwa na mabao 14 kwa jumla na kushikilia rekodi kwa muda hadi 2008. Shindano hili liliweza kuonyehwa katika runinga mara ya kwanza mwaka wa 1970 likiwa nchini Sudan,[3] ambayo iliweza kuchukua taji baaada ya kuwashinda Ghana- iliyokuwa ikicheza fainaili ya nne mfululizo.

1970: Muongo wa mabingwa

hariri

Kati ya mwaka 1970-1980 mataifa sita mbalimbali yaliweza kushinda : Sudan, Kongo-Brazzaville, Zaire, Moroko, Ghana, na Nigeria. Zaire ilishinda mara ya pili katika mwaka wa 1974 (ilishinda mara ya kwanza kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) baada ya kupambana na Zambia katika fainali. Kwa muda hadi sasa katika historia ya ushindani, hii ndio mechi ya kipekee ambayo imerudiwa baada ya timu hizo mbili kutoka sare 2-2 baada ya muda wa ziada. Finali hii ilichezwa siku mbili baadaye na Zaire kuibuka washindi kwa 2-0. Mchezaji wa mbele wa Zaire , Mulamba Ndaye alifunga bao zote nne za mechi hizo mbili: pia alikuwa alishikilia usukani kwa kuwa na mabao tisa katika msimu huo na kuweka rekodi ya mechi ya kibnafsi hadi wa leo. Miezi mitatu awali, Zaire ilikuwa taifa la kwanza la Afrika weusi kufuzu katika FIFA World Cup. Moroko iliweza kuchukua ushindi kwa mara yao ya kwanza katika ANC mwaka wa 1976 nchini Ethiopia na Ghana ilichukua ushindi mara ya tatu mwaka wa 1978,Katika mawka wa 1980 shindano hili lilifanyika Nigeria ambapo timu ya taifa ya Nigeria ililaza Algeria na kunyakuwa ushindi mara ya kwanza

1980: Kutawala kwa Kamerun na Nigeria

hariri

Ghana iliweza kunyakua ubingwa mara ya nne mwaka wa 1982 baada ya; kushinda Algeria katika nusu fainali katika muda wa ziada, na kupatana na Libya kama mwenyeji katika fainali. Hii mechi iliisha sare ya bao 1-1 baada ya dakika 120 na Ghana ilishinda katika penalti na kunyakuwa taji. Kamerun iliweza kuchukuwa taji la kwanza miaka miwili baadaye kwa kushinda Nigeria .Shindano la mwaka wa 1986ilikabiliana na Misri - watoro tangu fainali ya mwaka wa 1962 - Misri ilishinda kupituia penalti. Kamerun iliweza kushiriki katika fainali mara ya tatu mfululizo na kuchukua taji mara ya pili katika shindano la 1988hii ni baada ya kurudia kuchapa Nigeria mwaka wa 1984. Mwaka wa 1990, Nigeria ilipoteza nafasi ya kuchukua taji walipojiandikisha katika fainali mara ya tatu baada ya kujitokeza katika shindano hili mara nne na kupigwa na Algeria .

1990: Kuwasili kwa Afrika Kusini

hariri

Mwaka wa 1992 Kombe la Mataifa ya lilipanua mipaka na kuongeza idadi ya washiriki katika fainali ya shindano hili hadi 12; Timu hizi ziligawanywa katika makundi manne Kila kundi lilikuwa na timu tatu ambapo timu mbili za juu katika kila kundi zilifaulu katika robo fainali. Mjchezaji wa Ghana wa katikati kwa majina kiungo Abedi "Pelé" Ayew ambaye alifunga bao tatu, alitiwa taji la mchezaji bora wa shindano hili mwaka huo baada ya mchango wake kusaidia Ghana kufuzu fainali; hata hivyo alisimamishwa kucheza mechi hiyo na Ghana kushindwa na Ivory Coast katika mikwaju ya penalty ambako kila pande ilijaribu mara 11 ili kutambua timu itakayoshinda. Cote d'Ivoire waliweza kuweka rekodi katika shindano hili kwa kushinda mechi sita bila kufungwa bao.

Ule mpango wa timu 12, na tatu kila kundi kundi ulitumika tena miaka miwili baadaye, ambapo Tunisia iliyokuwa nyumbani iliwezwa kuondolewa katika shindano hili. Nigeria, ambayo ilifaulu katika Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia, ilishinda shindano hili baada ya, kuchapa Zambia, ambayo mwaka kabla ilipatwa na msiba wa maafa ambapo wengi wa wachezaji wao waliaaga dunia katika ajali ya ndege wakielekea katika mchuano wa kufuzu katika kombe la dunia. Mchezaji wa mbele kutoka Nigeria , Rashidi Yekini, aliyekuwa akiongoza kwa mabao wa 1992 aliweza kuongoza tena kwa mabao matano mwaka huo.

Afrika ya Kusini iliweza kuwa mwenyeji wa shindano la 20 la ANC mwaka wa 1996, na kushiriki katika shindano hili mara ya kwanza baada ya kupewa fursa ya kushiriki katika shindano hili walipoacha ubaguzi.Pia walikuwa wamejaribu mwaka wa 1994 lakini hawakufuzu. Idadi ya washiriki katika fainali iliongezeka hadi timu 16 ambazo ziligawanywa katika makundi manne. Hata hivyo, idadi halisi ya timu zilizocheza katika fainali mara ilikuwa15 tu kwani Nigeriailijiondoa katika shkindano hili dakika ya mwisho kwa sababu za siasa katika nchi yao. [11] Timu ya Bafana Bafana iliweza kushinda taji kwa mara ya kwanza kwa kuwalaza Tunisia. Nahodha wa Afrika Kusini Neil Tovey ndiye aliyekuwa mchezaji mzungu wa kwanza kuskika kile kikombe. [13] Afika Kusini ingeweza kufika fainaliwa miaka miwili baadaye nchini Burkina Faso, lakini hawakuweza kutetea taji lao kwani, iliweza kunyakuwa ushindi kwa mara ya nne.

2000: Ubingwa wa Kamerun ukifuatiwa na Misri

hariri

Toleo la 2000 liliweza kufanyika Ghana na Nigeria, badala ya Zimbabwe kwa kuwa ilitoka sare ya 2-2 baada ya muda wa ziada katika fainali, Kamerun ilishinda Nigeria katika penalti. Mwaka wa 2002,timu ya Indomitable Lions ilipokea taji mara ya pili mfululizo kama Ghana ilivyofanya katika miaka ya 1960 baada ya Misri kufanya vivyo hivyo mwaka 1957 na 1959. Kupitia penalti, ya Kamerun ilishinda Senegal ambayo ilikuwa mara yao ya kwanza kucheza fainali, ambayo pia ilipata kushika nafasi katika Kombe la ulimwengu baadaye mwaka huo. Timu hizi mbili zilizofika fainali waliweza kutolewa katika robo fainali nchini Tunisia ambapo timu ya nchi hii ilipokea ubingwa baada ya kuchapa Moroko 2-1 katika fainali. Shindano la 2006 lilishindwa na, Misri ambayo ilikuwa nyumbani.Iliweza kuweka rekodi ya bara kwa kuwa washindi mara tano. Shindano la 2008 lilifanyika Ghana ambapo Misri waliweza kutetea ubingwa wao na kunenepesha rekodi na ushindi wa sita baada ya kuwalaza Kamerun 1-0 katika fainali.

Baadaye

hariri

Kabla ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka wa 2008 vilabu vya ulaya viliomba kuwe na mabadiliko katika ratiba hiyo. Kwani shindano hili hufanyikan wakati sawa na michuano ya ulaya ambapo wachezaji wao wengi hawachezi kwani wako katika timu zao za nyumbani Katika Januari mwaka wa 2008, rais wa FIFA Sepp Blatter alitangaza kwamba yeye alitaka shindano kufanyika aidha Juni au Julai 2016, ilikuwa sambamba na kalenda ya kimataifa. Hii itasababisha shindano hili kutofanyika nchi nyingi katika Afrika ya kati na magharibi (kwani miezi hii huwa msimu wa mvua) na kama shindano hili litakuwa likifanyika miaka ilito sawa basi itabidi shindano hili kuskumwa katika miaka isiyo sawa ili kusiwe na mgogngano na shindano la kombe la dunia.

Fomati

hariri

Kufuzu

hariri

Tangu 1962 kumekuwa na michuano ya kufuzu katika fainali. Kutoka 1962-1990 michuano hii ilikuwa na mechi za kurudiwa, na idadi ya raundi ilitegemea idadi ya timu zinazoshiriki Kuanzia 1994 kuendelea timu ambazo zina azma ya kufuzu hugawanywa katika makundi na kucheza na kila timu katika kundi iliyowekwa Mpaka mwaka wa 2006 ambako timu ya nchi ambapo shindano hili litafanyika na mabingwa tetezi zilifaulupapo Kwanzia mwaka wa 2008 timu itakayo fanya shindano hili ndio wanafuzu papo hapo.Fomati ya kufuzu katika shinano hili imekuwa ikibadilikabadilika .Kwanzia mwaka wa 2008 timu 11 ndizo zinazofuzu katika fainali ambazo zinagawanya katika makundi ambayo yana timu nne na moja timu tatu. Timu zinazoshinda katika kundi ndizo zinafaulu na timu tatu zingine ambazo zina rekodi nzuri

Katika historia ya Kombe la Mataifa, kumekuwa na aina tatu za taji ambazo zimepatianwa .Kombe la kwanza mbalo lilikuwa la fedha, lilijulikana kama " Kombe la Abdelaziz Abdallah Salem ", ambalo ilikuwa jina lake rais wa kwanza wa kutoka Misri jenuari Abdelaziz Abdallah Salem. Baada ya ushindi wa tatu katika Kombe la Mataifa Ghana iliweza kumiliki kombe hilo mwaka wa 1978.[4]

Kombe la pili lilikuwa mwaka wa 1980-2000, na lilijulikana kama "nyara wa Umoja wa Afrika" au "African Unity Cup". [4] lilitolewa na Baraza Kuu la Michezo ya Afrika kwa CAF mwaka wa 1980 kabla ya mashindano na lilikuwa ni kipande mviringo na pete ya Olimpiki ambayo ililalia ramani ya bara ya Afrika na lilikuwa na vishikilio vya Triangle. Kamerun iliweza kumiliki kombe hili baada ya kuchukua ubingwa mwaka wa 2000.

Mwaka wa 2001,Toleo la tatu lilitokea, ambalo ni kombe la dhahabu lililoundwa nchini Italia. Kamerun, waliomiliki toleo la pili waliweza kuwa taifa la kwanza kushinda toleo hili.

Matokeo

hariri
mwaka Taifa mwenyeji Fainali Mechi ya nafasi ya Tatu
Mshindi Bao Nafasi ya pili Nafasi ya Tatu Bao Nafasi ya nne
1957   Sudan  
Misri
4-0  
Ethiopia
 
Sudan
  Afrika Kusini awe hana halali) (1)
1959   Egypt  
Misri
2-1 (2)  
Sudan
 
Ethiopia
(timu tatu tu walishiriki)
1962   Ethiopia  
Ethiopia
4-2
AET
 
Misri
 
Tunisia
3-0  
Uganda
1963   Ghana  
Ghana
3-0  
Sudan
 
United Arab Republic
3-0  
Ethiopia
1965   Tunisia  
Ghana
3-2
AET
 
Tunisia
 
Ivory Coast
1-0  
Senegal
1968   Ethiopia  
Congo DR
1-0  
Ghana
 
Ivory Coast
1-0  
Ethiopia
1970'   Sudan  
Sudan
3-2  
Ghana
 
United Arab Republic
3-1  
Ivory Coast
1972'   Cameroon  
Congo
3-2  
Mali
 
Kamerun
5-2  
Zaire
1974   Egypt  
Zaire
2-2 AET
2-0 Replay
 
Zambia
 
Misri
4-0  
Congo
1976   Ethiopia  
Moroko
1-1 (3)  
Guinea
 
Nigeria
3-2 (3)  
Misri
1978   Ghana  
Ghana
2-0  
Uganda
 
Nigeria
2-0 (4)  
Tunisia
1980'   Nigeria  
Nigeria
3-0  
Algeria
 
Moroko
2-0  
Misri
1982'   Libya  
Ghana
1-1 AET
(7-6) penalti
 
Libya
 
Zambia
2-0  
Algeria
1984'   Ivory Coast  
Kamerun
3-1  
Nigeria
 
Algeria
3-1  
Misri
1986'   Egypt  
Misri
0-0 AET
(5-4) penalti
 
Kamerun
 
Côte d'Ivoire
3-2  
Moroko
1988   Morocco  
Kamerun
1-0  
Nigeria
 
Algeria
1-1 AET
(4 - 3) penalti
 
Moroko
1990'   Algeria  
Algeria
1-0  
Nigeria
 
Zambia
1-0  
Senegal
1992'   Senegal  
Côte d'Ivoire
0-0 AET
(11 - 10) penalti
 
Ghana
 
Nigeria
2-1  
Kamerun
1994   Tunisia  
Nigeria
2-1  
Zambia
 
Côte d'Ivoire
3-1  
Mali
1996   South Africa  
Afrika Kusini
2-0  
Tunisia
 
Zambia
1-0  
Ghana
1998   Burkina Faso  
Misri
2-0  
Afrika Kusini
 
Congo DR
4-4 (5)
(4 - 1) penalti
 
Burkina Faso
2000   Ghana &
  Nigeria
 
Kamerun
2-2 AET
(4 - 3) penalti
 
Nigeria
 
Afrika Kusini
2-2 AET
(4 - 3) penalti
 
Tunisia
2002   Mali  
Kamerun
0-0 AET
(3 - 2) penalti
 
Senegal
 
Nigeria
1-0  
Mali
2004   Tunisia  
Tunisia
2-1  
Moroko
 
Nigeria
2-1  
Mali
2006   Egypt  
Misri
0-0 AET
(4 - 2) penalti
 
Côte d'Ivoire
 
Nigeria
1-0  
Senegal
2008   Ghana  
Misri
1-0  
Kamerun
 
Ghana
4-2  
Côte d'Ivoire
2010   Angola  
Misri
1-0  
Ghana
 
Nigeria
1-0  
Algeria
2012   Equatorial Guinea&
  Gabon
 
Zambia
0-0 AET
(8 - 7) penalti
 
Côte d'Ivoire
 
Mali
2-0  
Ghana
2013   South Africa  
Nigeria
1-0  
Burkina Faso
 
Mali
3-1  
Ghana
2015   Guinea ya Ikweta  
Côte d'Ivoire
0-0 AET
(9 - 8) penalti
 
Ghana
 
Congo DR
0-0 AET
(4 - 2) penalti
 
Guinea ya Ikweta
2017   Gabon
2019   Kamerun
2021   Cote d'Ivoire
2023   Guinea

(1) Mwaka wa 1957,   Afrika Kusini haikuruhusiwa kucheza kutokana na ubaguzi ubaguzi.
(2) Katika mwaka 1959, timu zile tatu zilicheza mara ingine mmoja. Katika mchezo wa mwisho wa michuano, Misri's ilipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Sudan kuwa mabingwa
(3) Hakukuwa na mechi na fainali rasmi mwaka wa 1976, kwani timu nne bora katika kila kundi ndizo zliwaania taji hili.
(4) Katika mwaka wa 1978, nafasi ya tatu ilinyakuliwa na Nigeria 2-0 baada Tunisia kujiuzulu wakiwa sare ya bao1-1 katika dakika 42.
(5) Hakukuwa na muda wa ziada .

Takwimu

hariri

Nchi zilizoshinda Michuano Mingi

hariri
 
Ramani wa idadi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika
N ° Ushindi Taifa Mwaka (s)
1 Mara 7   Misri 1957, 1959, 1986, 1998, 2006, 2008, 2010
2 Mara 4   Kamerun 1984, 1988, 2000, 2002
  Ghana 1963, 1965, 1978, 1982
4 Mara 3   Nigeria 1980, 1994, 2013
2 Mara 2   Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 1968, 1974
  Côte d'Ivoire 1992, 2015   Algeria 1990, 2020
6. Mara 1   Ethiopia 1962
  Sudan 1970
  Congo 1972
  Moroko 1976
  Afrika Kusini 1996
  Tunisia 2004
  Zambia 2012
  Senegal 2021

Nchi zilizocheza fainali Nyingi

hariri
7   Misri
  Ghana
6.   Kamerun
  Nigeria
3   Côte d'Ivoire
  Tunisia
  Sudan
  Zambia
  Algeria
2   Ethiopia
  Moroko
  Afrika Kusini
  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (mara moja kama   Zaire
1   Congo
  Mali
  Senegal
  Uganda
  Guinea
  Libya

Michuano kuonekana

hariri
Kushiriki Taifa
22   Misri
20   Côte d'Ivoire
19   Ghana
17   Nigeria
16   Kamerun
  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (mara moja kama   Zaire Congo-Kinshasa & Congo-Leopoldville)
  Tunisia
  Zambia
15   Algeria
  Moroko
12   Senegal
10   Ethiopia
  Guinea
9   Burkina Faso (mara moja kama   Upper Volta)
8   Mali
  Afrika Kusini
  Sudan
7   Angola
  Togo
6.   Congo
5   Gabon
  Kenya
  Uganda
4   Msumbiji
3   Benin
  Libya
2   Liberia
  Malawi
  Namibia
  Niger


  Sierra Leone
  Zimbabwe

1   Botswana
  Cabo Verde
  Guinea ya Ikweta
  Morisi
  Rwanda
  Tanzania

Nchi ambazo shindano hili limehudhuriwa kwa wingi

hariri
Majeshi Taifa Mwaka (s)
Mara 4   Misri 1959, 1974, 1986, 2006
  Ghana 1963, 1978, 2000 ^, 2008
Mara 3   Ethiopia 1962, 1968, 1976
  Tunisia 1965, 1994, 2004
Mara 2   Sudan 1957, 1970
  Nigeria 1980, 2000 ^
Mara 1   Kamerun 1972
  Libya 1982
  Côte d'Ivoire 1984
  Algeria 1990
  Moroko 1988
  Senegal 1992
  Afrika Kusini mwaka wa (1996).
  Burkina Faso 1998
  Mali 2002
  Angola 2010
  Mali 2012 ^
  Guinea ya Ikweta 2012 ^

Mengine baadaye majeshi:

  Moroko (2015)
  Libya (2017)
  • ^ Co-majeshi

Wachezaji walio na bao nyingi

hariri
Mabao Scorers
18   Samuel Eto'o
14   Laurent Pokou
13   Rashidi Yekini
12   Hassan El-Shazly
11   Patrick Mboma,   Hossam Hassan
10   Ndaye Mulamba,   Didier Drogba,   Joel Tiéhi,   Mengistu Worku,   Francileudo Santos,   Kalusha Bwalya
9   Abdoulaye Traoré
8   Manucho,   Ahmed Hassan,   Wilberforce Mfum,   Pascal Feindouno
7   Flávio,   Roger Milla,   Taher Abouzaid,   Ali Abo Greisha,   Frédéric Kanouté,   Jay-Jay Okocha,   Benni McCarthy,   Christopher Katongo
6   Mayanga Maku,   Mohamed Aboutreika,   George Alhassan,   Abedi Pele,   Ahmed Faras,   Julius Aghahowa,   Segun Odegbami,   Shaun Bartlett
5   Lakhdar Belloumi,   Rabah Madjer,   Djamel Menad,   Jean-Michel M'Bono,   Hosny Abd Rabo,   Mohamed Ad-Diba,   Mohamed Nagy "Gedo",   Amr Zaki,   Emad Moteab,   Asamoah Gyan,   Fantamady Keita,  Seydou Keita,   Muda Lawal,   Peter Odemwingie

Wachezaji walio na bao nyingi kwa mwaka

hariri
mwaka Player Mabao
1957   Diab Mohammed Diab El-Attar (Ad-Diba) 5
1959   Mahmoud Al-Gohari 3
1962   Abdelfatah Badawi
  cadowga Worku
3
1963   Hassan El-Shazly 6.
1965   Ben Acheampong
  Osei Kofi
  Eustache Manglé
3
1968   na Laurent Pokou 6.
1970   Laurent Pokou 8
1972   Salif Keita 5
1974   Mulamba Ndaye 9.
1976   Keita Aliou Mamadou 'N'Jo lea' 4
1978   Philip Omondi
  Opoku Afriyie
  Segun Odegbami
3
1980   Khaled Al Abyad Labied
  Segun Odegbami
3
1982   George Alhassan 4
1984   Taher Abouzaid 4
1986   Roger Milla 4
1988   Lakhdar Belloumi
  Roger Milla
  Abdoulaye Traoré
  Gamal Abdelhamid
2
1990   Djamel Menad 4
1992   Rashidi Yekini 4
1994   Rashidi Yekini 5
mwaka wa (1996).   Kalusha Bwalya
  Marko Williams
5
1998   Hossam Hassan
  Benedict McCarthy
7
2000   Shaun Bartlett 5
2002   Patrick Mboma
  René Salomon Olembe
  Julius Aghahowa
3
2004   Patrick Mboma
  Frédéric Kanouté
  Youssef Mokhtari
  Jay-Jay Okocha
  Francileudo dos Santos
4
2006   Samuel Eto'o 5
2008   Samuel Eto'o 5
2010   Gedo 5
2012   Pierre-Emerick Aubameyang
  Cheick Diabaté
  Didier Drogba
  Christopher Katongo
  Houssine Kharja
  Manucho
  Emmanuel Mayuka
3
2013   Emmanuel Emenike
  Wakaso Mubarak
5

Mkuu Takwimu

hariri
Pos. Timu Kushiriki Mshindi Pili Tatu Nne P W D L Pts. NI GC Tofauti
1   Misri 22 7 1 3 3 90 51 15 24 168 154 84 +70
2   Nigeria 17 3 4 7 0 86 46 21 19 159 122 81 +41
3   Ghana 19 4 4 1 3 83 46 16 21 154 111 71 +40
4   Kamerun 16 4 2 1 1 71 37 20 14 131 110 67 +43
5   Côte d'Ivoire 20 1 2 4 2 81 36 19 26 127 120 90 +30
6   Zambia 16 1 2 3 0 64 26 18 20 96 79 66 +13
7   Moroko 15 1 1 1 2 57 19 22 16 79 66 54 +12
8   Tunisia 16 1 2 1 2 60 19 22 19 79 76 75 +1
9   Algeria 15 1 1 2 2 60 20 18 22 78 69 72 -3
10   Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 16 2 0 1 1 59 16 18 25 66 68 84 -16
11   Senegal 12 0 1 0 3 46 15 11 20 56 52 46 +6
12   Mali 8 0 1 2 3 40 15 11 14 56 51 56 -5
13   Afrika Kusini 8 1 1 1 0 35 14 12 9 54 42 35 +7
14   Guinea 10 0 1 0 0 35 11 12 12 45 52 51 +1
15   Sudan 8 1 2 1 0 24 7 6 11 27 28 38 -10
16   Ethiopia 10 1 1 1 2 27 7 3 17 24 29 61 -32
17   Angola 7 0 0 0 0 23 4 10 9 22 29 37 -8
18   Congo 6 1 0 0 1 22 5 6 11 21 21 34 -13
19   Burkina Faso 9 0 1 0 1 32 4 9 19 21 29 55 -26
20   Gabon 5 0 0 0 0 15 5 4 6 19 15 21 -6
21   Togo 7 0 0 0 0 22 3 7 12 16 17 36 -19
22   Libya 3 0 1 0 0 11 3 5 3 14 12 13 -1
23   Uganda 5 0 1 0 1 16 3 1 12 10 17 31 -14
24   Kenya 5 0 0 0 0 14 1 4 9 7 8 24 -16
25   Guinea ya Ikweta 1 0 0 0 0 4 2 0 2 6 3 5 -2
26   Zimbabwe 2 0 0 0 0 6 2 0 4 6 8 13 -5
27   Cabo Verde 1 0 0 0 0 4 1 2 1 5 3 4 -1
28   Liberia 2 0 0 0 0 5 1 2 2 5 5 7 -2
29   Rwanda 1 0 0 0 0 3 1 1 1 4 3 3 0
30   Malawi 2 0 0 0 0 6 1 1 4 4 6 11 -5
31   Sierra Leone 2 0 0 0 0 5 1 1 3 4 2 11 -9
32   Namibia 2 0 0 0 0 6 0 2 4 2 9 18 -9
33   Msumbiji 4 0 0 0 0 12 0 2 10 2 4 26 -22
34   Tanzania 1 0 0 0 0 3 0 1 2 1 3 6 -3
35   Niger 2 0 0 0 0 6 0 1 5 1 1 8 -8
36   Benin 3 0 0 0 0 9 0 1 8 1 4 20 -16
37   Morisi 1 0 0 0 0 3 0 0 3 0 2 8 -6
38   Botswana 1 0 0 0 0 3 0 0 3 0 2 9 -7

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. http://news.bbc.co.uk/sport2/hi/football/africa/cup_of_nations/1709599.stm
  2. news.bbc.co.uk. "African Nations Cup - How it all began". BBC. Iliwekwa mnamo 9 Machi 2007.
  3. 3.0 3.1 news.bbc.co.uk. "The early years". BBC. Iliwekwa mnamo 9 Machi 2007.
  4. 4.0 4.1 news.bbc.co.uk. "Nations Cup trophy revealed". BBC. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2007.

Masomo zaidi

hariri

Viungo vya nje

hariri