Ramani
uwakilishi wa kuona wa nafasi ya dhana; taswira inayosisitiza uhusiano kati ya vipengee vya nafasi fulani, kama vile vitu, maeneo au mada.
(Elekezwa kutoka Map)
Ramani ni picha - kwa kawaida mchoro - ya dunia au sehemu au sifa zake.
Ni tofauti na picha iliyopigwa kwa kamera kutoka ndege au chombo cha angani kwa sababu mchora ramani anachagua anachotaka kuonyesha na kuzipa uzito sifa anazotaka kuziwekea mkazo.
Kuna aina nyingi za ramani:
- ramani za topografia huonyesha sura ya nchi (kwa mfano: bahari, nchi kavu, milima, mito, kimo cha ardhi na kina cha bahari)
- ramani za idadi huonyesha sifa fulani kuhusiana na dunia (kwa mfano: historia, uchumi, mtawanyiko wa wakazi katika nchi n.k.)
- ramani inaweza kufuata sura ya nchi
- ramani inaweza kufuata mahitaji ya msomaji (ramani ya njia ya reli huonyesha mstari tu na mfuatano wa vituo bila kutaja kona na mabadiliko ya mwelekeo)
Kila mchoraramani anahitaji kuchagua jinsi ya kuonyesha mambo yake. Kwa ramani za kijiografia tatizo hutokana na umbo la dunia ambalo ni tufe wakati ramani kwa kawaida ni karatasi bapa.
Viungo vya nje
hariri- International Cartographic Association (ICA) (Kiingereza)
- Mwongozo wa Jiografia na Ramani (Kiingereza)
- The History of Cartography Project (Kiingereza)
- Mapping History Project - Chuo Kikuu cha Oregon (Kiingereza)
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|