Marangu ni mji ulioko katika Mkoa wa Kilimanjaro. Neno "Marangu" linamaanisha mahali penye vijito vingi vya maji. Mji huu ni kati ya maeneo maarufu nchini Tanzania.

Lango la kuingia Kilimanjaro National Park.
Maporomoko ya Maji ya Marangu.
Marangu.

Historia hariri

Kabla ya uhuru mwaka 1961, mji wa Marangu ulikuwa makao makuu ya wilaya ya Vunjo iliyokuwa chini ya (Mangi Mwitori) Petro Itosi Marealle na (Mangi Mkuu) Thomas Marealle, aliyepewa ufalme mwaka 1951, ambaye aliishi katika mji wa Moshi.

Uchumi hariri

Wakazi wengi wa Marangu ni wakulima wa ndizi, mboga za majani na kahawa. Hata hivyo, chanzo kikuu cha mapato ni utalii kutokana na Mlima Kilimanjaro na vivutio vingine.

Elimu hariri

Shule mbalimbali na vyuo, kama vile Chuo cha Ualimu cha Marangu na Shule ya Wasichana ya Ashira, viko katika mji huu vikitoa huduma kwa wanafunzi toka maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Tazama pia hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Marangu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.