Marumaru
(Elekezwa kutoka Marble)
Marumaru (pia: marmar - kutoka Kiarabu مرمر; kwa Kiingereza: marble) ni mwamba wa gange uliobadilika kutokana na joto na shindikizo ndani ya ganda la dunia katika kipindi cha miaka milioni kadhaa. Kikemia ni hasa CaCO3.
Ni jiwe gumu sana linalopatikana katika rangi mbalimbali.
Hupendwa sana kama jiwe la ujenzi, hasa kama ni nyeupe. Kama ni haba katika eneo fulani hutumiwa kama mapambo tu, kama vile kwa kufunika kuta.
Jiwe lenye rangi mbalimbali hutumiwa kwa sakafu katika majengo muhimu au kama mapambo ya kuta za ndani.
Tangu kale marumaru ilitumiwa pia kwa kuchonga sanamu.
Tovuti za nje
- Inlaid marble Ilihifadhiwa 18 Julai 2016 kwenye Wayback Machine.
- Tips for cleaning marble Ilihifadhiwa 10 Agosti 2007 kwenye Wayback Machine.
- Learning to carve by Marc Levoy.
- Marmo Qarry in the Massa-Carrara region, Italy
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Marumaru kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |