Mariana Ochoa

Mariana Yolanda Ochoa Reyes (amezaliwa tar. 19 Februari 1979, katika mji wa Mexico City, Mexico) ni muigizaji wa filamu na pia mwanamuziki kutoka nchi ya Mexico.
Pia alikuwa mwanachama wa kundi la muziki maarufu kama OV7 (Lilifahamika kama La Onda Vaselina wakati lilianza shughuli zake). Baada ya hapo ikawa kama bahati kwa OV7 kuachana na Ochoa katika kundi na Ochoa kuanza kujitangaza mwenyewe katika masuala ya muziki na uigizaji.

Mariana Ochoa
Jina la kuzaliwa Mariana Yolanda Ochoa Reyes
Alizaliwa 19 Februari 1979
Mexiko
Jina lingine Mariana Ochoa
Kazi yake Mwigizaji
Mwanamuziki

Wasifu

Maisha ya filamu na muziki

Tamthilia yake kwanza kumpa umaarufu na kukubalika kwa Mariana ilikuwa La Hija Del Jardinero, iliyo andaliwa na TV Azteca production. Tamthilia hiyo ilipokelewa vizuri tu huko Latini Amerika.

Hivi karibuni Mariana alitoa tamthilia nyingine nzuri ya kuvutia iitwayo "Amor Sin Condiciones" na kuweza kuipiku hata ile ya 'Secreto de Amor' ambayo iliandaliwa mwaka 2001 na kampuni ya Venevisión wakishirikiana na Fonovideo ya Miami nchini marekani.

Pamoja Ochoa na kushughulika na kurekodi albamu yake ya pili lakini bado pia anashughulika na kurekodi tamthilia mpya itakayo rushwa hewani na TV Azteca, tamthilia inaitwa "Se Busca un Hombre" ambayo pia inaandaliwa na kampuni ya TV Azteca.

Albamu alizotoa

Albamu Mwaka Studio
Yo Soy 2004 EMI Music
Luna Llena 2007 Warner Music


Mnamo mwezi Machi, 2006, Ochoa amebadilisha studio ya EMI na kuhamia Warner Music kwa mkataba wa kurekodi kwa muda wa miaka kumi.
Mwezi Julai, 2007, Ochoa alirekodi albamu yake ya pili iliyoitwa Luna Llena.

Nyimbo Zenye Umaarufu

  • My Lover
  • Deseos
  • Qué Importa
  • Me Faltas Tú (#20 - EXA Guatemala
  • Aunque No Estés (Kwa Ushirikiano wa Alex Ubago)

Marejeo

  1. http://www.emimusic.com.mx/portal/hgxpp001.aspx?2,114,23,O,S,0,MNU;E;72;7;MNU;
  2. "Como Nunca Existió"
  3. http://foro.univision.com/univision/board/message?board.id=mariana_ochoa&message.id=78515
  4. Ochoa Kwenye 10 Bora

Vioungo vya nje

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mariana Ochoa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.